google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 14, 2018

Ukishindwa Kuzingatia Mambo Haya Mawili Tu, Utakwama.

No comments :

Kila mtu anapanda kwenye ngazi ya mafanikio yake. Kila mtu anakimbilia ngazi ya mafanikio yake, pasipo kujali ni kitu gani ambacho anakifanya, lakini kila mtu yupo kwenye ngazi ya kuelekea kwenye mafanikio yake kwa namna fulani hivi.
Tatizo la watu wengi wanapokuwa wanapanda ngazi ya mafanikio yao, badala ya kwenda juu wanakua ni watu ambao wanapanda ngazi hiyo kwa kushuka chini. Unaweza usinielewe kiurahisi, lakini ndivyo watu wanavyofanya hivyo.
Yapo mambo ambayo kwa kawaida huwa yanachangia katika watu hao badala ya kupanda ngazi ya mafanikio kwa kwenda juu na wao wanakwenda chini. Mambo haya naweza yakawa yanafahamika kwa wengi au yasifahamike kwa namna yoyote ile.
Lakini jambo mojawapo ambalo linaweza likafanya mtu badala ya kupanda ngazi yake ya mafanikio na hadi kuweza kufanikiwa, anajikuta anarudi nyuma  hio yote ni kutokana na matumizi ya muda wake. Muda unaoutumia unautumia vipi.
Ni watu wengi sana ambao matumizi ya muda wao hayajakaa sawa. Mara nyingi sana watu hawa hawafanyi vitu vya kuwasaidia kulingana na muda wao walionao. Ni watu wa kufanya sana vitu vinavyowakwamisha na kuwarudisha nyuma kimafanikio.

Ni hatari sana na ni ngumu kuweza kupanda ngazi ya mafanikio na kuweza kufanikiwa kama matumizi yako ya muda unayatumia kwa vitu ambavyo si sahihi yaani vitu vinavyoukwamisha na kukurudisha nyuma.
Kuutumia muda wako hivyo hiyo ni sawa na kuamua kurudisha mafanikio yako kwa kurudi nyuma. Unaweza ukawa unaona unapanda ngazi ya mafanikio yako vizuri, kumbe unaigiza yaani unarudi nyuma kimafanikio.
Unatakiwa ujue namna ya kutumia muda wako vizuri sana ili uweze kupanda ngazi yako ya mafanikio kwa ufasaha na kuweza kufanikiwa.  Kama utakuwa unatumia muda wako hivyo tu kila wakati ujue kabisa unajiangusha wewe kwa kurudi nyuma.
Jambo la pili, ambalo linaweza likafanya upande ngazi yako ya mafanikio kwa kushuka chini badala ya kwenda juu ni nguvu zako. Inatakiwa ifike mahali utambue nguvu zako unazitumia kwenye mambo gani.
Haiwezekani kufanikiwwa kama nguvu zako unazielekeza sana kwenye mambo ambayo hayawezekani yaani mambo ya hovyo. Ni vyema kutumia nguvu zako kwenye mambo ambayo yanakupa mafanikio na sio kinyume cha hapo.
Kama unaona kuna jambo linakupotezea nguvu zako, bila kujali nguvu zako ni za kufikiri au kusema, lakini kama linakupotozea nguvu zako na wewe hufaidi na kitu chochote, nakushauri sana achana na jambo hilo mara moja kwani halikufai.
Watu wenye mafanikio hawapotezi nguvu zao hovyo, ni watu wa kuhakikisha wanatumia nguvu zao kwa ufasaha mkubwa sana. Na wewe unaweza ukawa ni miongoni mwao ukatumia nguvu zako vizuri na zikakusadia kufanikiwa.
Kwa namna yoyote hutakiwi kupote nguvu zako kwa kitu kinachokuridisha nyuma. Unatakiwa sana kuchunga nguvu zako na zikatumika vizuri kwa manufaa ya mafanikio yako makubwa ya leo na ya kesho pia.
Kitu cha kuzingatia hapa ni kwamba, ukishindwa kuzingatia mambo haya mawili yaani matumizi yako ya muda na matumizi yako ya nguvu zako, ujue utashindwa tu. Ni lazima kujua umuhimu wa kutumia nguvu zako na muda wako vizuri sana.
Haya mambo mawili ndiyo yanayowapa watu  mafanikio sana, nimesema muda na matumizi ya nguvu zako. Ukiwachunguza watu waliofanikiwa wanatumia muda na nguvu zao vizuri, watu hawa hawapotezi muda wao au nguvu zao kwa namna yoyote ile.
Kuanzia sasa, anza kutumia muda wako vizuri na anza pia kutumia nguvu zako vizuri. Usifanye vitu ambavyo vitakupotezea muda na nguvu zako. Haya ni mambo ya muhimu sana na kwenye mafanikio yako na vitakusaidia kufikia kwenye kilele cha mafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.