google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 2, 2018

Hakikisha Kitu Hiki Kisikuzuie Kabisa Kufikia Mafanikio Yako.

No comments :
Haijalishi kwenye safari yako ya mafanikio unakutana na ugumu wa aina gani, lakini unachopaswa kuelewa ugumu huo unaokutana nao ni ugumu wa muda mfupi sana kwako na wala hauhitaji wewe kukata tamaa.
Uelewe hivi, pamoja na kwamba unakutana na ugumu ili hali unaweka juhudi za kutosha, unapaswa kuvumulia na kuendelea kuweka juhudi tena kwani matunda ya mafanikio utakayoyapata yatakuwa ni ya muda mrefu kwako.
Ni rahisi kufikiri au kuamua kuachana na ndoto zako na kutoa sababu mbalimbali kwa sababu ya ugumu ambao unakutatana nao kimaisha. Hayo yote hayawezi kukusaidia unachotakiwa kujua ugumu huo ni wa muda na wewe unatakiwa kupambana.
Kesho yako unatakiwa kuitengeneza wewe kwa kufanya kila linalowezekana hadi kuweza kufanikiwa. Kutoa sababu kwa sababu mambo ni magumu hilo sio suluhisho hata kidogo, unatakiwa kukazana tu bila kujali nini kinakutokea.
Labda nikulize kitu? Ni kipi unachokipenda upate mateso ya muda halafu baadaye uje ufurahie maisha yako kwa muda mrefu au upate starehe za muda na baadaye uje uteseke. Naamini utachagua bora ya mateso ya muda mfupi.
Kama iko hivyo na kwako, hutakiwi sasa kukatishwa tamaa na hali unayokutana nayo. Ugumu wa maisha usikuchanganye hata kidogo. Kila mtu aliyeko duniani amekutana na ugumu wa maisha kwa wakati wake yeye, hakuna ambaye hajakutana na ugumu.
Wafatilie watu wote wenye mafanikio, utajua ni watu ambao wamekutana sana na ugumu wa maisha. Kile unachokiona kwa nje ni picha tu za mafanikio unayoyaona kwa nje, lakini ndani mwao wamekutana na magumu mengi sana.
Najua hawawezi kukwambia jinsi ilivyo, lakini ukweli uko hivyo. Ndio maana tunasema, unatakiwa ukabiliane sana na ugumu wa kila aina yoyote ile hadi uweze kufanikiwa, kwani hali hiyo ni ya muda tu, nayo itapita.
Uwe unalala chini, uwe unakula mlo mmoja kwa siku, uwe huna pesa kabisa, yote hayo ipo siku yataisha ikiwa utakuwa ni mtu wa kuishi kwa malengo na kuchukua hatua za kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua.
Inawezekana pia njia unayopita sasa hivi inakuchanganya kwa sababu ya taabu zake nyingi na imekuwa kama njia ya miiba na kuona mbele tumaini limekufa. Unatakiwa kujiambia mafanikio ni lazima hata kitokee kitu gani.
Maisha ya mafanikio hayaji mara moja, ni matokeo ya mabadiliko ya hatua kwa hatua hadi kufikia mafanikio. Kipi kinakushinda na kwa nini una wasiwasi, kwa nini uumie na ugumu wa maisha ulionao, kila kitu kinabadilika ukiamua.
Unachopaswa kufanya ni kuchukua hatua za haraka kila wakati. Hutakiwi kusita sita, chochote unachotaka kukifanya, kifanye. Acha kudharau kitu, chukua hatua za kufanya na hapo ndio utakuwa unabadilisha maisha yako.
Kabla siku hii ya leo haijakwisha unatakiwa kuelewa kukubali kukabiliana na changamoto, weka juhudi, pambana na ugumu wa maisha na itafika wakati ugumu huo utakwisha na utakuwa na maisha bora kwako.
Kwa jinsi utakavyokuwa ukiweka juhudi kukabiliana na hali uliyonayo, ndivyo utakavyokuwa ukibadilisha maisha yako na kuyafanya kuwa bora. Usikate tamaa, ugumu wa maisha usikuzuie kabisa kufikia mafanikio yako.
Hakuna kitu au hali yoyote ambayo inakuzuia kufanikiwa hata kama hali hiyo kwako ni ngumu kwako. Kila changamoto kwenye maisha ni ya muda tu. Ni wakati wa kuamua kusonga mbele na  siku zote usiruhusu ugumu wa maisha ukakuzuia kufanikiwa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.