google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 23, 2018

Huu Ndio ‘Ugonjwa’ Mpya Hatari Usipothibitiwa Mapema, Utaangamiza Familia Nyingi.

No comments :
Inafahamika yapo magonjwa mengi sana, ambayo yamekuwa tishio kwa familia na jamii inayotuzunguka kwa muda mrefu. Magonjwa hayo yapo ambayo yamekuwa yana dawa na yapo ambayo hayana dawa, lakini yapo.
Kwa kuwa mimi si daktari hapa katika makala haya sitataja sehemu ya magonjwa hayo ambayo yamekuwa ni hatari kwa familia, pengine na taifa kwa ujumla, bali hapa mimi nitazungumzia ugonjwa mmoja tu ambao naufahamu ila ni hatari sana.
Ugonjwa huu ambao nauzungumzia hapa na ambao ikiwa hauathibitiwa mapema, basi tujiandae kupoteza familia nyingi na kuzipeleka kubaya zaidi, ni ugonjwa wa mmonyoko wa maadili, ndio nimesema ni mmonyoko wa maadili.
Kwa miaka ya hivi karibuni ukifatilia kwa makini, utagundua swala la kuporomoka kwa maadili kadri siku zinavyokwenda mbele nalo limekuwa likiongezeka kwa kasi. Watoto wa sasa, wamekuwa  si watoto wa miaka ile, mambo yamekuwa yametofautina sana.

Malezi bora kwa watoto yanatakiwa kusimamiwa vizuri.
Hilo unaweza ukaliona vizuri kwa watoto wa sasa, kama si wa kwako basi wa jirani na kama si wajirani basi ni wa ndugu. Lakini kitu ambacho kipo na kinaendelea kutokea katika jamii zetu tunamoishi kila siku.
Najua walezi wa watoto kama wazazi, walimu pia ambao kwa sehemu wanajukumu la kukaa na watoto kwa muda mrefu, hapa wanaweza wakawa wananielewa kwa uzuri sana kwamba mmomonyoko wa maadili tayari limekuwa ni tatizo au ugonjwa ambao unakuja kimya kimya.
Kwa bahati mbaya sana kila mtu anakazana na kinga ya nyumbani kwake na wengine hata hiyo kinga hawaijui, matokeo yake watoto wanakuwa wanalelewa tu kama kibahati, na mwisho wa siku ni hatari kubwa ambayo inapelekea mmonyoko wa ukweli.
Kiuhalisia ukiangalia  yapo mengi yanayosababisha ‘ugongwa’ huu wa mmonyoko wa maadili kwa sasa kutokea kwa kasi kuliko wakati mwingine. Moja ya msingi mbovu inaweza ikawa ni malezi mabovu ya wazazi na walezi kwa watoto na hata pia mitandao ya kijamii.
Hivi ni vitu ambavyo vinaweza vikawa na mchango mkubwa sana kupelekea mmonyoko wa maadili kwa watoto wetu. Na pasipo vitu hivi au swala hili la mmomonyoko wa maadili kudhibitiwa basi taifa la kesho tutakalokuwa nalo litakuwa ni bovu sana.
Unaona mpaka hapo ni jukumu la kila mmoja wetu kusimamia kwa umakini swala la mmonyoko wa maadili kutokuendelea, vinginevyo tutakuwa na taifa ambalo litakuwa halina maadili kwa siku za huko baadae.
Ni imani na mategemeo yangu wazazi na walezi watajitahidi kuziba mianya yote inayopekeleka mmonyoko wa maadili. Hayo yote hayawezi kufanikiwa pasipo kutoa ushirikiano kwa wazazi wote.
Pia walimu wetu inatakiwa washirikishwe na watiwe moyo na wazazi katika kuhakikisha watoto wanalelewa katika maadili mazuri na bora. Kila mtu akisimama katika nafasi yake mabadiliko yatawezea kutokea.
Lakini ikiwa tukishindwa kuthibiti kwa sasa mmomonyoko wa maadili, basi tujiandae kuwa na kizazi ambacho kitakuwa  kipo kipo tu. Mpaka hapo ieleweke hatujachalewa, uwezo wa kuthibiti ‘ugonjwa’ huu wa mmonyoko wa maadili inawezekana.
Inawezekana unajiuliza tunaanzia wapi, anzia hapo ulipo, ‘mtoto wa mazazi mwezio ni mtoto wako pia.’ Kama unaona mtoto amekosea kitu hata kama sio wako, chukua jukumu la kumuonya.
Pale mtoto atakapogundua alaa kumbe anaweza kuonywa na mzazi ambaye si wake, najua atajirekebisha na vivyo hivyo tutajikuta tuna kizazi chema, kizazi ambacho tutakifurahia siku za usoni kwenye maisha yetu.
Watengenezaji wa maisha ya watoto wetu ni sisi wenyewe, jukumu ni letu sote. Tuchuke hatua za kuweza kubadili sisi kwa kuwa wazazi au wazazi wawajibikaji na kwa kufanya hivyo tutaweza kuthibi ‘ugonjwa’ huu wa mmonyoko wa maadili.
Fanyia kazi ujumbe huu, linda kizazi cha kesho kwa kukipa maadili bora na ya manufaa leo na si kesho.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.