google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 1, 2018

Kama Unataka Kuwa Mfanyabiashara Mwenye Mafanikio Hakikisha Una Kuwa Hivi.

No comments :
Katika sayari hii  idadi kubwa ya shughuli ambazo hufanywa na mwanadamu ni biashara, kama ndivyo hivyo basi naomba niweze kujikita zaidi katika kulizungumzia jambo hilo siku ya leo. Na siku ya leo nataka kusema jambo moja ambalo kila mfanyabishara anapaswa kulifahamu ili kujikuza katika biashara yake.
Na jambo hilo  wafanyabiashara walio wengi wamekuwa wakilitumia kinyume chake hata kupelekea wao wenyewe kutokufanya vizuri katika tasnia ya biashara. Wengi wa wafanyabiashara wanafikiria kufanya hivyo ni kukua kibiashara kumbe si kweli.
Japo hilo si lingine bali  kusema uongo juu ya biashara ambazo wanazifanya. Jambo hili limekuwa likiwafanya wateja wengi kuhama na kwenda sehemu zingine, na kitendo hicho  hufanya mfanyabiashara kupoteza wateja bila ya yeye mwenyewe kujijua.
Na kutoka na uongo ambao wanautumia wafanyabiashara wengi wamekuwa , vinara wa kulalama ya kwamba vyuma vimekaza, huku wao wenyewe ndio chanzo cha kukuza kwa vyuma hivyo kwani wamekuwa wakiwafukuza wateja hao njia ya udanganyifu.
Inawezekana ukawa bado hujanielewa ipo hivi, hivi hujawahi kununua kitu fulani  huku mfanyabiashara aliyekuuzia kitu hicho akikukwambia kitu hicho ni original, ila baada ya kukitumia kitu hicho ukakikuta ni feki? Hivi hujawahi kula chipsi za jana huku mfanyabiashara wa chipsi akakwambia hizi ni za leo leo. Bila shaka umewahi kukutana na uongo wa aina hii.
Kwa athari ambazo ulikutana nazo mara baada ya kununua vitu hivyo ukiwa kama mteja , swali linakuja je unadhani je? unadhani utakwenda kununua kitu kilekile kwa yule ambaye alikuuzia hapo awali? Bila shaka hakuna ambaye atadiliki kufanya hivyo.
Swali linakuja ni nini Kifanyike?
Binafsi nadhani lipo jambo la muhimu ambalo kila mfanyabiashara anapaswa kulifahamu hasa pale anapofanya biashara yale na jambo hilo sio jingine bali ni kuwa muwazi wa wateja wake. Kuwa muwazi kwa wateja wako hukufanya ukue kibiashara na kufanya kuongezeka kwa wateja.
Unapoingia katika fungu la kuwa mfanyabiashara muongo fahamu fika unapoteza wateja wako. Kumueleza mteja ukweli kuhusu bidhaa au huduma unayoitoa kunakufanya uweze kudumu katika biashara yako na kumiliki wateja kwa muda mrefu.
Hivyo ndugu yangu kama kweli unataka kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio ni vyema ukachagua fungu lililo jema kwako kwa kuamua kuwa ni mtu wa kusema ukweli katika biashara ambayo unaifanya. Kama kitu ni origino basi uwe unamaanisha.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Ndimi; Afisa mipango Benson chonya

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.