google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 27, 2018

Fursa Za Kunufaika Nazo Katika Ufugaji Wa Kuku.

1 comment :

Rafiki, fursa zipo nyingi ambazo zinatokana na ufugaji wa kuku leo naenda kukueleza fursa ambazo zitakusaidia wewe kukua zaidi kiuchumi huku ukiwanufaisha jamii kubwa ya watu ulionao katika maeneo yako na taifa kwa ujumla.

Rafiki tumejifunza mambo mengi kuhusu ufugaji wa kuku kila kitu unachopasa kukijua kuhusu ufugaji wa kuku tayari umekijua sasa ni wakati wa utekelezaji tu na siyo maneno tena kwa sababu mafanikio yanatokana na hatua sahihi unazochukua.
                           
Unapoweka mipango ya kufuga kuku usiishie tu kupanga kufuga kuku mia au kuku elfu moja usiishie kufuga tu fikiria kufuga na kuzalisha mayai yakutosha kwa ajiri ya kuboresha afya kwa jamii kubwa ya watu wanaotuzunguka.


Kwa Tanzania bado upo mkubwa wa mayai hasa mayai ya asili ni adimu sana hebu rafiki amka uikoe jamii kubwa ya watanzania wanaokosa mayai kwa ajili ya chakula, kwani uhitaji bado ni mkubwa.

Kunielewa vizuri ngoja nikwambie kitu rafiki najua unafahamu kuwa mimi ni mfugaji na pia unafahamu kuwa nilikuwa natangaza kuhusu watu wanaohitaji mayai, lakini kwa sasa hata sitangazi tena kuhusu mayai kwa sababu mahitaji ya watu ni makubwa.

Watu wamekuwa wakiweka oda kwa zaidi ya wiki tatu wote hao wanahitaji mayai nashindwa kuwafikia wateja wote kwa wakati uhitaji umekuwa mkubwa kuliko uzalishaji nimekuwa nikiwasiliana na wazalishaji mbalimbali ambao wanafuga kuku lakini hawajawa na uhakiki wa mayai.

Kwa wakati sahihi sasa nimefikilia kuzalisha mayai kwa wingi ambayo yatakuwa yana uwezo wa kuwafikia wengi zaidi kwa wakati, Rafiki panga na wewe kuwa sehemu ya watu watakao nufaika na mradi huu wa kuku.

Nakupendekezea kwako rafiki tumia njia ya sayansi katika kupunguza gharama ya chakula cha mifugo yako, ongeza uzalishaji wako, lifikie soko kubwa zaidi, na hapo utakuwa na uhakika mkubwa wa kipato chako.

Pia  ngoja nikwambie jambo rafiki , iwapo utafanya ufugaji wako kwa kutumia sayansi yakupunguza gharama ya chakula basi utafanya ufugaji wako kwa gharama ya chini sana baada ya kuuza kwa bei kubwa wewe uza kwa bei ya kawaida tu.

Kama sokoni mayai ya asili yanauzwa mia tano wewe uza kwa mia tatu hadi mia nne kwa sababu gharama za uendeshaji kwako zitakuwa chini sana ukilinganisha na wafugaji wengi ambao wanafuga bila kutumia sayansi hii.

Unaweza ukajiuliza kwanini mayai ya kisasa yanauzwa bei ya chini na mayai ya asili (kuku chotara) yanauzwa bei ghari? je jibu nikiwa na  mayai ya asili ni adimu kupatikana ndio maana bei yake ni kubwa ukilinganisha na mayai ya kisasa.

Naomba nikuulize rafiki nani mkombozi wa jambo hili siyo mwingine ni mimi na wewe tunajukumu la kuzalisha mayai kwa wingi yawe ya kisasa au ya asili bado yanahitajika sana kwa jamii yetu mimi  nimeanza wewe je?

Weka mipango yako sawa wewe rafiki usifikirie kuishi kufuga kuku wachache fikiria kuwa na matawi kubwa ya mayai, fikiria kusambaza mayai Tanzania nzima,  mayai yanahitajika siyo nasema uongo.

Jambo lingine utakalo nufaika nalo ni kuwa na oda nyingi kutoka sehemu mbalimbali kama vile mahotelini, kwenye mighahawa, kwenye vibanda yya chipsi, majumbani, maofisini na maeneo mengine mbalimbali.

Kwa leo nimekupa mwanga tu wa fursa za kunufaika nazo kutokana na ufugaji wa kuku. Na ukumbuke tumeongelea fursa moja tu ambayo ni kufungua matawi ya uuzaji wa mayai kwa wingi sana. Je, fursa ipi inafata itokanayo na ufugaji wa kuku? Tukutane wiki ijayo katika somo linalofuata.

Ni mimi wako katika ufugaji, 
FRANK MAPUNDA,
0656 918 243.

1 comment :

  1. niko sumbawanga naweza kuwapataje
    tafadhali nijibu kwa email yangu
    gikaroh48@gmail.com

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.