google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 21, 2018

Huu Ndio Ukweli Kuhusu Maisha Ya Mafanikio Unaotakiwa Kuufahamu Vizuri.

No comments :

IIi kufikia mafanikio, kuna wakati inatakiwa uujue ukweli wa aina fulani hivi na kwa kuujua ukweli huo utakusaidia kufanikiwa. Lakini kuendelea kuishi kwa kujidanganya na huku ukiwa hujui mbele wala nyuma juu mafaniko utajidangaya tu, hutafanikiwa.
Najua utaweka juhudi hii au ile kufikia mafanikio, lakini hutaweza kufikia kwa sababu utakuwa bado unaishi kwenye dunia ya giza ambayo inakuwa imekufunika na ushindwe kutafuta mafanikio yako kama inavyotakiwa iwe kwako.
Kupitia makala hii ya leo, tunakuangazia kweli tano ambazo unatakiwa uzijue na ili zikusaidie kufanikiwa. Ni matumaini yangu, utafaidika vya kutosha na kuweza kubadilisha maisha yako kwa kufanyia kazi kweli hizi. Kweli hizi ni zipi, karibu ujifunze.

1. Ni kazi ngumu kufikia mafanikio.
Asije akakudanganya mtu kwamba kufikia mafanikio ni kazi rahisi, huyo atakuwa ni mtu mwongo kabisa. kufikia mafanikio inahitaji uweke juhudi na maarifa ya kutosha ili kufikia mafanikio hayo. Kama huweki juhudi huwezi kufanikiwa.
Kwa lugha nyepesi tu bila kukuficha kitu naomba nikwambie kufikia mafanikio ni kazi ngumu na sio nyepesi kama wengine wanavyowezza wakawa labda wanakudanganya kwamba ni kitu rahisi tu na cha mara moja.
Lakini hata hivyo haimaanishi kwa kuwa ni kazi ngumu kufika mafanikio, basi haiwezekeni kuyafikia. Kufikia mafanikio ni kweli ni kazi ngumu, lakini inawezekana kuyafikia kwa asilimia zote na hilo halina ubishi. Huu ni ukweli unaotakiwa uumeze kama ulivyo bila kutema.
2. Unahitaji msaada kufikia mafanikio.
Hakuna mafanikio ambayo unaweza ukayapata ukiwa wewe kama wewe. Unahitai msaada ili kuweza kufikia mafanikio yako. Pasipo kuweza kupata msaada huwezi kupata mafanikio yoyote, kwani mafanikio yapo kwa watu.
Kwa hiyo utaona unahitaji msaada kutoka kwa rafiki zako, utahitaji msaada kutoka kwa ndugu zako wa karibu na hata pia utahitaji msaada kutoka kwa wale watu wanaokusaidia kazi zako na ambao wanakuwa wana mchango fulani kwako.
Huhitaji hapa kutunisha kifua kusema mimi ndio mimi, mafanikio ni muunganiko wa misaada tofauti tofauti kutoka kwa watu wengine pia. Ukweli huu unatakiwa kuujua kwamba mafaniko yanahitaji msaada wa wengine pia, hivyo heshimu watu.
3. Makosa ni ngazi ya kufikia mafanikio.
Imezoeleka kati ya kitu kinachowaangusha wengi katika safari ya mafanikio ni yale makosa ambayo wanakuwa wanayafanya wakati wanatafuta mafanikio yao. Watu hao wamekuwa wakisahau kwamba makosa ni kama shule.
Unapokuwa unatafuta mafanikio ya aina fulani, kukosea ni kitu cha kawaida sana. Kwa hiyo hutakiwi kujilaumu kwa chochote kwamba kwa nini umekosea katika eneo la aina fulani, badala yake unatakiwa ujifunze kusonga mbele.
Utakwama sana kwenye maisha yako, kama makosa utakuwa unayachukulia  kwa umakini sana na inakupelekea mpaka kushindwa kufanya vitu vingine. Yafanye makosa yawe shule yako ya kukuwezesha wewe kuweza kusonga mbele zaidi na si kukurudisha nyuma.
4. Kuwa king’ang’anizi.
Sifa mojawapo kubwa ya watu ambao wamefanikiwa ni wabishi. Ni watu ambao hawakubali kushindwa kirahisi, ni watu ambao wanaamua liwalo na liwe, lakini wanapigana mpaka kuhakikisha ndoto zao zinaweza kutimia.
Hata wewe ili uweze kufanikiwa unatakiwa uwe king’ang’anizi sana. Kwa kifupi unatakiwa uwe na roho ngumu, roho ambayo haikubali kushindwa kirahisi, inayotaka lazima mabadiliko yaweze kutokea kwenye maisha yako.
Ukiujua vyema ukweli huu kwamba unatakiwa kuwa mbishi hilo litakusaidia sana kuweza kuweza kung’ang’ana kufanya kila linalowezekana na kuongeza juhudi zote kwa kufanya kila kilicho cha msingi, ilimradi tu ufanikiwe.
5. Jipe hamasa ya mafanikio kila siku.
Usifanye kosa la kusubiri hali au kitu chochote kikupe hamasa ya kufanya kile unachotaka kufanya. Jipe hamasa hiyo wewe mwenyewe kila siku. Kama huoni hamasa ikitokea usitulie, wewe endelea kufanya, hamasa itakuja mbele ya safari wakati unaendelea.
Washindi katika mafanikio hawasubiri hamasa ili kuweza kusonga mbele. Ni watu wa kufanya na mwisho wa siku hamasa inayofuata. Kwa hiyo hata wewe unaweza ukaanza kujihamasisha wewe mwenyewe.
Hakikisha unafanyia kazi kweli hizi muhimu kwako na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.