google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 20, 2018

Usitegemee Kufanikiwa Kama Hautafanya Jambo Hili Mapema.

No comments :
Kufanya maandalizi ya kitu chochote kile ni jambo la muhimu sana kwako na pia ni moja ya dalili nzuri kwamba unajiandaa kuwa mshindi kwa kitu hicho unachokifanya. Kama haufanyi maandalizi ni rahisi tu kushindwa na hilo halina ubishi.
Ndio maana unaona mwanafunzi ni lazima ajiandae mapema ili aweze kufaulu mtihani wake, ndio maana unaona mkulima anaandaa shamba lake mapema pia ili wakati wa kilimo ukifika ili aweze kufanikisha kilimo chake.
Hiyo haitoshi unaona pia, mwana riadha anaanza kufanya mazoezi mapema  ya kukimbia ili wakati ukifika aweze kushinda mbio hizo, hiyo yote inaonyesha maandalizi ni kitu cha muhimu sana kwa ushindi wowote ule.
Hakuna mshindi anayetokea au kuibuka tu kiholela pasipo kuwa na maandalizi yale ya mwanzo ya kuweza kujifua haswaa ili kutengeneza ushindi huo. Kila ushindi unaouona umetokezea kwa nje, ujue kabisa ushindi huo umeandaliwa na haujaja kwa bahati.
Unapaswa ukumbuke pia hata wakati ule wa Nuhu. haikuwa kipindi cha mvua au gharika wakati Nuhu anajenga safina, bali Nuhu alifanya maandalizi ya mapema na gharika inayokuja mbele yake na hilo kweli lilikuja kutokea.

Halikadhalika na wewe unatakiwa kujenga maisha yako kwa ubora sana kipindi ambacho mambo yako hayajaanza kuharibika au mambo hayajaanza kubanana na mpaka ukasombwa na gharika ya changamoto.
Unatakiwa kujua kwamba wakati wa kutengeneza maisha yako ni sasa wakati bado una nguvu za kutosha ni si baadae. Huu ndio wakati wa kutengeneza safina ya maisha wakati hali, nguvu na muda wako bado vinakuruhusu.
Kitafika kipindi ambacho hautakuwa na uwezo huo yaani muda utakuwa huna, na wala nguvu utakuwa huna. Angalia sana usije ukaanza kulia kama wale watu waliokuwa wakimlilia Nuhu wafungulie kwenye safina, lakini akawaambia hakufunga yeye mlango.
Hata wewe angalia usije ukafika muda ambao utaanza kuwalilia watoto wako, ukaanza kuwalilia wajukuu wako wakati utakapoanza kusombwa na maji na ukiangalia ulishindwa kujenga safina yako mapema. Wakati wa kufanya na kukazana ni sasa na si kesho.
Kwa nini usubiri mabaya ya kukute ili upambane nayo wakati una uwezo wa kujindaa sasa mapema na kuyaepuka. Huhitaji kusubiri kitu, unahitaji kufanya kitu kwa ajili ya maisha yako ya kesho bila kujali hli uliyonao kwa sasa ni ipi.
Hebu nikuulize kitu, kama utashindwa kutengeneza maisha yako sasa na yakaonekana yana maana, je, utaweza kweli ukishazeeka. Hapo ulipo ni kijana umeshindwa je, ikifika uzeeni utaweza? najua hutaweza hata ufanyaje.
Ndio maana unatakiwa kuweka juhudi sana za kuhakikisha unafanya kila kinachowezekana wakati bado damu yako ina chemka, wakati bado una nguvu ili ufanikiwe. Nikwambie tu ukisubiri, jiandae kusombwa na gharika ya changamoto za maisha.
Na ubaya wa gharika inakuwa haina msamaha au hakuna kupona, ikikukuta ujue ndio tayari umeshaenda. Kwa hiyo usikubali kupoteza maisha yako ya mafanikio kwa sababu ya kushindwa kufanya maandalizi mapema.
Kuanzia sasa fanya maandalizi mapema kwa kila kitu ambacho unachokifanya. Usipofanya maandalizi mapema utaanguka na utajiangusha wewe mwenyewe na kutakuwa hakuna mtu ambaye ataweza kukuamsha tena.
Ndiyo maana, unatakiwa uweke akiba mapema kipindi ambacho kabla hujaishiwa. Unatakiwa uzime moto mapema, kabla moto haujawaka vya kutosha. Ni muhimu kufanya maandalizi mapema ya chochote kile ukifanyacho ili ikusaidie kuwa mashindi.
Kama hautafanya maandalizi ya mapema kwa chochote unachokifanya kushindwa hautaweza kukwepa hata kidogo. Kumbuka hata Nuhu alijenga safina mapema, kabla hata gharika haijafika. Tafakari na chukua hatua.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.