google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 8, 2018

Mbinu Itakayokusaidia Kuwa Karibu Na Wateja Wako Ni Hii.

No comments :
Miongoni mwa changamoto ambazo huwakabili wafanyabiashara wengi ni kuwapoteza wateja wengi bila wao kujua. Na tatizo hilo huanza kutokana na wafanyabiashara hao kutokuwa na mawasiliano thabiti kati yao na wateja.
Kwa kutambua hilo Siku ya leo nitakupa mbinu itayaokusaidia kuwa karibu na wateja wako. Na mbinu hii endapo utaamua kuitumia itakusaidia sana katika biashara unayoifanya.
Nasema hivi nikiwa nina ushahidi wa kutosha kwani mimi binafsi mbinu hiyo imenisaidia kuweza kuwa karibu na wateja wangu na hatimaye naona matunda yake.  Ni mbinu ambayo inafanya kazi vizuri sana ukiitumia.

Na mbinu hiyo siyo nyingine bali ni kuwa na mawasiliano thabiti baina yako na wetaja wako au kwa lugha ya kitaalamu huitwa ‘customer database’. Customer database ndiyo ambayo hutumiwa na makampuni mbalimbali.
Kwa mfano makampuni  ya simu hutumia mbinu hii ili kumjuza mteja ujio wa bidhaa, punguzo la bei, au kumjuza mteja taarifa muhimu kuhusu huduma husika. Kwa hiyo taarifa zote za mteja zinakuwa hapo.
Na kwa kufanya hivi kumewafanya wateja kupata taarifa sahihi na kwa muda sahihi  kuhusu huduma ambayo hutolewa na kampuni husika. Mteja anakuwa hakosi taarifa sahihi kwa sababu anakuwa anatumiwa mara kwa mara.
Kwa kuliona hili nimeona ni vyema nawe ukatumia mfumo wa aina hii ili uwe karibu na wateja wako, mawasiliano thabiti huweka ukaribu baina na wateja wako, hii haijalishi ni biashara gani ambayo unaifanya.
Bali kitu cha muhimu cha kuzingatia ni kuhakikisha unafanya hivyo ili uwe unawajuza wateja wako kuhusu biashara unayoifanya. Kama kuna mabadiliko yeyote yanayayohusu biashara yeyote unayoifanya basi usisite kuwajuza wateja wako.
Jinsi ya kuandaa mfumo wa mawasilino wa wateja wako (customer database)
Mfano;

JINA LA MTEJA
NAMBARI ZAKE ZA SIMU
BARUA PEPE YA MTEJA
MAHALI ANAPOISHI
1.
BENSON CHONYA
0757-909942
bensonchonya23@gmail.com
KIMARA-DSM
2
IMAN NGWANGWALU
0713-048035
dirayamafanikio@gmail.com
LUSHOTO-TANGA
3
XXXXX
06XX-XXXX
XXXXX@gmail.com
MIYOMBONI-IRINGA
 Hivyo ndivyo muundo wa 'customer database' ambavyo unatakiwa kuwa.
ANGALIZO: KUMBUKA MAWASILIANAO HAYO YAWE KWA AJILI YA BIASHARA TU, ENDAPO UTAIFANYA VINGINEVYO KUMBUKA LOLOTE LINAWEZA KUKUTOKEA.
Fanyia kazi mfumo huo wa ‘customer data base’ ili uwe na msaada kubwa kwako na kumbuka pia kuchukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako afisa mipango wa mafanikio yako,
Benson Chonya,
Mawasiliano; +255 757-909942,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.