google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 17, 2018

Hii Ni Hatua Muhimu Sana Katika Mafanikio Yako, Unatakiwa Uifanyie Kazi Kikamilifu.

No comments :
Najua kabisa kuna vitu ambavyo hapo ulipo tayari umeshafanya hata kama ni vidogo sana lakini umefanya. Hivyo vitu vinaonyesha kuna hatua ambazo tayari umeshachukua ndio maana upo hapo.
Huwezi kusema wewe hapo ulipo hujachukua hatua yoyote, kila mtu anachukua hatua ya aina fulani kwenye maisha yake, hata kama hatua hiyo ni ya kurudi nyuma lakini hatua hiyo tayari imeshachukuliwa.
Watu wengi wanakwama kwenye maisha kwa sababu tu ya kuishia kwenye zile hatua ambazo tayari wameshachukua na kusahau hatua moja ya muhimu sana kwao. Hatua hii ndiyo ambayo mimi na wewe tunatakiwa kuichukua kila wakati ili kufanikiwa.
Moja ya hatua muhimu sana kwenye maisha yako unayotakiwa kuichukua na ambayo naizungumzia hapa ni hatua inayofuata au unaweza kuiita ‘next step’ ikiwa utaamua kutumia lugha ya watu. Watu wengi wanashindwa kupiga hatau kwa sababu ya kusahau hatua hii.
Utakuta mtu alikuwa na mipango fulani na kweli kaifanikisha. Kutokana na kuifanikisha mtu huyu anajisahau na kuridhika sana na pale alipo na kusahau hatua inayofuata baada ya hapo ni hatua gani ambayo ni muhimu zaidi kwake.
Kwa sababu unatakiwa ujue ukishafanikiwa katika jambo la kwanza,  hatua inayofuata kwako ni hatua gani? Pasipo kujua hatua inayofuata yaani ‘next step’ huwezi kusogea na utajikuta unaanza kufanikiwa kwa kwenda nyuma badala ya mbele.
Kama nilivyokwambia maisha ya wengi yamekwama kwa sababu ya kusahau hatua inayofuata ni ipi. Ni kweli ulitafuta kazi umepata, hatua sasa inayofuata hapo ni nini? Kama una ndoto za kubaki hapo kwenye hiyo kazi milele ujue kabisa umesahau ‘next step’ yako.
Unaposhindwa kujua ni nini ufanye ili kuboresha kazi yako na maisha yako kwa ujumla, kwa kuzingatia hatua inayofuta unatakiwa ujue unajiangusha wewe mwenyewe. Huwezi kusonga mbele kimafanikio kama unasahau hatua inayofuta au huizingatii.
Hatua inayofuata inatengeneza muunganiko kati ya hatua ulizochukua tayari  na kule unakotaka kwenda. Kama unakuwa huchukui hatua inafyofuata ujue kabisa utaanza kuporomoka katika kufanikiwa kwako.
Mafanikio makubwa yanatengenezwa na wale watu ambao wako tayari kuchukua hatua inayofuata, pasipo kujali hatua inayofuata ni ndogo au kubwa kiasi gani. Kikubwa unatakiwa kuchukua hatua nyingine baada ya hatua ya kwanza kukamilika.
Wajasiriamali wanaofikia ndoto zao na kuwa wafanyabiashara wakubwa kabisa, ni watu ambao kila wakati wapo tayari kuchukua hatua inayofuata. Kuhusu hilo wanalijua na wanaelewa umuhimu wa kuchukua hatua inayofuta.
Kuanzia sasa unatakiwa ujue kwamba hata kama umefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, lakini ipo hatua inayofuata kwako. Hatua hiyo ni muhimu sana kwa sababu itakufikisha tena kwenye mafanikio mengine makubwa zaidi ya hapo.
Ukiona unashindwa kuchukua hatua inayofuata, kinachofuata kwako hapo baada ya muda usishangae sana mafanikio yako yakaanza kuporomoka kwa kasi kubwa sana kwako. Kuchukua hatua inayofuta ni jambo la lazima kwako.
Huu ni wakati kwako wa kuchukua hatua inayofuata baada ya hatua ya kwanza ambayo umeifanikisha imekamilka. Unatakiwa kujiuliza hatua yako ya pili ni ipi, ambayo inafuata baada ya hiyo, ukiijua hatua ya inayofuata haraka sana chukua hatua pasipo kusita kitu.
Utatengeneza maisha ya mafanikio ikiwa utajua namna ya kutumia hatua inayafuata. Ukumbuke pia hii ni hatua muhimu sana kwa mafanikio yako unayoyatafuta. Anza kujenga ushindi mkubwa maisha yako kwa kuchukua hatua inayofuata.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.