google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 6, 2018

Usikubali Mambo Haya Yakuzuie Kufanikiwa.

No comments :
Yapo mambo mengi ambayo yanaweza yakawa chanzo cha kushindwa kwetu. Kwa leo nitakutajia mambo mawili tu, nimeamua kuyataja hapa kwa sababu ndio mambo ambayo yanawazuia watu wengi sana kushindwa kuweza kufanikiwa.
Ukiwatazama watu wengi ambao wameshindwa ndani mwao wanayo sana mambo hayo na ambayo wanakuwa wanayashikilia sana na unakuta inakuwa ndio chanzo cha anguko lao la kushindwa kuweza kufikia mafanikio.
Jambo la kwanza ni hofu. Watu wengi wamekuwa wakikwama kwenye maisha yao kwa sababu ya hofu kubwa. Hofu hii imekuwa ikiwazuia kuchukua hatua na wakati mwingine hofu hii imekuwa ikiwazuia hata kuthubutu kuchukua hatua ndogo ndogo.
Kwa kawaida unapokuwa na hofu sana huwezi kufanya kitu kwani kila kitu unakuwa unaogopa hali ambayo inapelekea wewe inakuwa ni ngumu sana kuweza kufanikiwa kwako mpaka pale utakapokuwa umeziweka hofu pembeni.

Umeshawahi kujiuliza au kutambua ni kwa jinsi gani ambavyo hofu zako zinavyochangia katika kukuangusha wewe. Kama ulikuwa hujui kuanzia sasa unatakiwa ujue hilo kwamba hofu inaweza ikakuzuia ukashindwa kufanya mambo mengi sana.
Unatakiwa kuachana na kila aina ya hofu na kisha kuvaa moyo wa kijasiri ambapo utaweza kukabiliana na vitu vingi na ukashinda. Ikiwa hautafanya hivyo utazidi kuwa mtu wa kushindwa sana maishani mwako.
Hakuna mshindi katika maisha ambaye amejawa na hofu za kupitiliza. Ni jukumu lako wewe kuanzia sasa kuhakikisha kwanza hofu unaziweka pembeni ili kusonga mbele. Ukiweka hofu pembeni, jiandae kuanza kuwa mshindi wa mafanikio yako.
Jambo la pili ni kukatataliwa. Inatakiwa uelewe kukatliwa kunakuwa kunauma sana pale unaporuhusu kukataliwa huko kukuumize. Mtu anapokwambia hapana, haimaanishi yeye ndiye yupo sahihi, hata yeye anaweza asiwe sahihi kabisa.
Usione vibaya kile unachokifanya kinapokataliwa kwa namna moja au nyingine. Tafuta njia au majibu kwa nini kitu hicho kinakataliwa. Unapopata majibu hayo inabidi yakusaidie kuweza kuendelea mbele zaidi.
Lakini kuchukua hatua ya kusikitika sana na kuanza kujiona yaani wewe ndio hufai eti kwa sababu kuna mtu amekukatalia utakuwa unajikosea wewe. Kumbuka kuchukulia kukataliwa huko kama fundisho kwako na si vinginevyo.
Chunga sana kila wakati mambo haya mawili yasikuzuie wewe kuweza kuchukua hatua za kuweza kufanikiwa. Usikubali hofu na wala usikubali kukataliwa kwa namna yoyote ile ndio kukazuia safari yako ya mafanikio.
Usiwe miongoni mwa watu ambao wanashindwa kwa sababu ya kuzuiliwa na hofu na kukataliwa. Washindi katika maisha wanajua vizuri namna ya kukakabiliana na mambo hayo na hadi kuweza kushinda na kufikia ngazi ya juu kimafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.