google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 4, 2018

HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Maelezo Marefu, Mwisho Huleta Uongo.

No comments :
Habari rafiki na karibu katika wakati mwingine wa kuweza kujifunza hekima za maisha na mafanikio kama ilivyo kawaida ya siku yetu ya leo. Kupitia hekima hizi zinatupa nafasi ya sisi kujifunza mambo ya kale kwa upya kabisa na tofauti.
Huwezi kutoka vile vile ikiwa utakuwa unajifunza hekima hizi, kwani zitakusaidia wewe kuyaangalia maisha yako kwa jicho la kitofauti. Sasa nikukaribishe uchukue kalamu na karatasi na ukaribie jamvini ili tuweze kujifunza kwa pamoja.

1. Mtu anayehamisha mlima, anaanza na jiwe moja.
Hakuna kinachoshindikana kwenye maisha ikiwa wewe utaamua sasa kwamba ni nini unakitaka. Yawe ni matatizo ukitaka yaondoke yataondoka au uwe ni mradi fulani, ukitaka kuufanya utaufanya na utakupa matokeo.
Hekima hii inatuonyesha na inatutaka tuwe wavumilivu na kujua kwamba kila kitu kinaweza kubadilika kikipewa muda. Ndio maana hekima inasema hata mtu ayetaka kuhamisha mlima huwa anaanza na jiwe moja.
Kwa hiyo hata wewe usizuiliwe na kitu chochote, anza kuhamisha jiwe moja moja kwa chochote kile unachokifanya na itafika utafanikiwa. Usitishike na ukubwa wa mlima ulionao, anza kuhamisha wewe jiwe moja moja na mafanikio utayaona.
2. Watu ndio muhimu, vitu vingine tunavipata tu.
Katika hekima hii ya maisha na mafanikio inatuonesha unaweza ukapoteza pesa ukaipata, unaweza ukapoteza kitu chochote kile na ukakipata, lakini si kupoteza mahusiano au watu wako wa karibu na  wenye msaada.
Msisistizo wa hekima hii unaonyesha, ni muhimu kutunza mahusiano bora ya watu na si kuyapoteza hovyo hovyo, kwani kupoteza kabisa mahusiano hayo linakuwa ni jambo la hatari ambalo linatufanya tuishi kama kisiwa.
Mahusiano bora ndio msingi mkubwa wa mafanikio yetu pia. Inapotokea ukawa ni mtu wa kupotezea watu na kuthamini vitu, hiyo kwako unakuwa unajiweka kwenye hatari. Unapaswa kukumbuka kwamba watu ni muhimu,  vingine tunavipata tukiweka juhudi.
3. Maelezo marefu, mwisho huleta uongo.
Kila mmoja anapaswa kujua anatakiwa kuwa mtu wa kutokutoa maelezo marefu sana kwa kitu ambacho kinaeleweka. Inatakiwa kueleza kitu kwa ufasaha na ikaeleweka pale kinapotakiwa na watu wakalitambua hilo.
Katika hekima hii, inatuonyesha kwa uwazi kwamba, maelezo marefu mwisho wa siku huleta uongo. Ni jukumu lako kujua pale unapaonza kujielezea sana kupitiliza ujue uongo unaweza ukafata hapo.
Hilo unaweza ukaliona kwa watu waongo ni kipi wakifanyacho. Watu waongo mara nyingi wanatumia maelezo marefu sana kama sehemu ya kutetea uongo wao. Hivyo, tunaambiwa malezo marefu mwisho wa siku huleta uongo, tafakari.
Fanyia kazi hekima hizi na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.