google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 7, 2018

Kifanyie Sana Kazi Kitu Hiki Kikupe Mafanikio.

No comments :
Ni kiwango gani cha imani uliyonayo juu ya mafanikio yako? ni kiwango gani cha thamani unachotoa juu ya mafanikio yako au ni kiwango cha juhudi unazozielekeza kwenye mafanikio yako, hivyo vyote vinategemea na wewe.
Nimesema hivyo vyote vinategemea na wewe kwa sababu, vipaumbele unavyoviweka katika mambo hayo niliyoyataja, ukiongeza na hatua unaziweka siku hadi siku, ni matokeo ya wewe kufanyia kazi mambo hayo ambayo unaamini yatakupa mafanikio.
Ndio maana unapoona mwanamuziki, daktari, mwanamichezo au injinia wa kitu chochote kile amefanikiwa sana, hayo yote hayaji kwa bahati mbaya ni matokeo ya yeye kuweza kufanyia kazi kitu hicho anachokifanya.
Mafanikio unayoyaona kwa mtu yoyote yanakua ni matokeo ya kufanyia kazi imani aliyonayo juu ya mafanikio yake, matokeo ya kufanyia kazi thamani anayotoa kila siku na pia ni matokeo ya kufanyia kazi juhudi zake za kila siku.

Ni rahisi sana kuweza kusema mimi nakwenda kufanya hiki au kitu kile, lakini linapokuja swala la kuweka kazi tena kila siku  ili uweze kufanikiwa hapo ndipo watu wengi wanakuwa wanakimbia na kupishana na mafanikio yao kabisa
Unachopaswa kujua na kuelewa, kwa kile unachokifanya haijalishi ni kidogo kiasi gani, unatakiwa kukifanyia kazi na kujifunza kupitia hicho haswa yaani unatakiwa kuwa mtaalamu wa kitu hicho ndani nje, kitakupa mafanikio.
Unapokuwa unafanyia kazi kitu hicho ambacho unakifanya, uwe na uhakika mkubwa ni lazima utavuna matokeo makubwa ambayo yataweza kukusaidia sana kufikia mafanikio mkubwa maishani mwako.
Tatatizo la watu wengi, hawako tayari kufanyia kazi kiuhakika yale mambo wanayoyafanya. Utakuta ni watu ambao wako nusu nusu sana kwenye mambo ambayo wanafanya utafikiri sio mambo yao.
Unapokuwa uko hivyo na ukategemea labda muujiza utoke ili ufanikiwe, kitu hicho hakiwezi kutokea siku moja. Hiyo iko hivyo kwa sababu, mafanikio hayaendi kwa bahati, mafanikio yanaenda kutokana na wewe kufanyia kazi mambo yako.
Hapo ulipo unaweza ukajiuliza una ndoto gani? Je, ndoto hizo unazifanyia kazi kwa kuweka juhudi? Je, ndoto hizo unazifanyia kazi kuchukua hatua kila siku? Kama unafanya hivyo uko salama, lakini ikiwa kinyume chake ni maumibvu andika.
Usikubai maisha yako tena yakaendelea kuwa magumu kwa sababu ya wewe kushindwa kufanyia kazi ndoto zako. Chukua hatua hata kidogo sana kuma hatua kubwa zinakushinda kuchukua.
Safari kwa kawaida ni safari tu, ilimradi umeianza. Hata wewe katika safari yako ya mafanikio unatakiwa kuzifanyia kazi ndoto zako karibu kila siku. Usipofanya hivyo kama nilivyosema muda utafika utakwama.
Kuna msemo mmoja unasema ‘ukitaka kuhamisha mlima, anza na jiwe moja’. Ndicho kitu na wewe unatakiwa kukifanya. Anza kufanyia kazi ndoto zako kwa kuhamisha jiwe moja moja na itafika siku utashangaa mlima umeondoka kabisa.
Usivurugwe wala kuchanganywa na maisha kwa namna yoyote ile. Kikubwa kwako ambacho nataka kusema hapo kwako ni umuhimu wa kukifanyia kazi yale malengo uliyonayo tena kila siku iitwapo leo.
Katika hili hutakiwi kuwa na visingizio hata kidogo. Fanyia kazi ndoto zako kila siku hata kama inafika wakati umebanwa au huna nafasi kabisa. unaweza kujikumbusha kabisa malengo yako kwa kuyaandika mahali na yakakupa hamasa ya kufanya zaidi.
Unapaswa kujua hivi, unapofanyia kazi ndoto zako kila siku, hiyo ni nafasi pekee kubwa ambayo inakufanya uikaribie ndoto hiyo na mwisho utafika kwenye mafanikio unayoyataka. Kitendo cha kufanyiakazi jambo unalolifanya, ni kitu cha msingi sana katika mafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.