google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 6, 2018

Hili Ndilo Jambo Mojawapo Linawafanya Matajiri Kuzidi Kufanikiwa Sana.

No comments :
Zipo siri ambazo matajiri wanazijua na ndizo ambazo zinawafanya wawe matajiri. Na wewe siri hizo kwa sababu, huna ndio maaana unaendelea kubaki hapo ulipo. Ukumbuke hata hivyo matajiri hawabahatishi wanajua siri ya mafanikio yao ilipo.
Na moja ya siri ambayo ni ya kawaida tu, ambayo wewe na mtu mwingine anaweza kuitekeleza na kuifata na ikapampa mafanikio ni siri ya kutoa. Sio utani bali ni ukweli wa wazi matajiri ni wa watu wa kutoa sana ulinganisha na watu wa kawaida.
Na maskini hawatoi sio kwa sababu hawana kitu, bali ni kama tabia zao. Na kitendo cha kutokutoa tena huko ni sawa na kuongeza umaskni mwingine ambao huwafanya wabaki pale pale na zipo hasara za kutokutoa tena kubwa.

Naona kuna mwingine ananishangaa na kusema sasa mimi nitatoa nini wakati sina kitu. Nikuulize tu labda hivi wewe unayefikiria hivyo, ni nani aliyekwambia ili utoe ni lazima uwe na pesa. Unatakiwa utoe kile ulichonacho na sio ambacho hauna.
Katika kutoa huko ndiko unafungua milango mingi sana ya baraka, lakini kama hutoi pia unajifungia milango mingi  ya mafanikio yako  na unakua unashangaa sasa mbona maisha yako yanakwama sana na huelewi hata ufanyaje.
Ipo miujiza katika utoaji. Kama wewe ni mtu wa dini unaweza ukanielwa zaidi lakini kwa hapa nitakwambia kitu kimoja tu ambacho, ukiwa ni mtoaji mzuri hata jicho la tatu, jicho la fursa ni lazima utakuwa nalo.
Kama umejenga tabia ya kutoa bila kutegemea kupokea basi jiandae na vile vile kupokea fursa na mambo makubwa pasipo hata wewe kutegemea, hiyo ni kanuni na iko hivyo, ikiwa ina maana kwamba kile unachotoa, kitakuja kwako kwa njia nyingi.
Ikiwa unataka kupokea kitu fulani ni kwanza lazima ujue kutoa, vinginevyo utakosa asilimia kubwa sana ya mambo au vitu vyako. Usiwaze kufanikiwa sana kama wewe si mtoaji. Watu wenye mkono wa birika rafiki yangu hawafaniiwi unatakiwa kujua.
Huhitaji kujibana bana, tafuta vingi na toa pale unapoona kwako panafaaa. Kama usipotoa huwezi kuona mengi yanayokuzunguka ikiwemo pamoja na fursa kama nlivyokwambia. Unataka mafanikio makubw ni lazima ujifunze na kutoa pia.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,








No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.