google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 25, 2018

Usipoteze Muda Na Nguvu Zako Kwa Kitu Hiki Kidogo.

No comments :
Ni upotevu wa muda na nguvu nyingi sana kama kila wakati unaamua kuweka nguvu zako katika kulaumu watu wengine kwa kile ambacho kinatokea. Kama wewe ni mtu wa lawama, elewa kabisa unapoteza muda na nguvu zako bure.
Kwa jinsi ilivyo unavyokuwa unalaumu, maanake unashugulika na tukio ambalo kiuhalisia limeshapita. Kwa hiyo hapo unakuwa ni sawa na mtu ambaye unaelekeza nguvu zake nje ya kitu ambacho hakisaidii sana.
Kitu cha msingi kwako na ambacho kitakusaidia si wewe kundelea kuchukua lawama, kama ni makosa ni tayari yameshatokea, unachotakiwa wewe ni kuweza kuchukua hatua  za kusonga mbele na si lawama zako ambazo hazina msingi.
Tafuta namna gani utakavyo weza kundelea mbele na si kutafuta ni kwa namna gani kulaumu udhaifu wa watu wengine kwa muda mrefu. Maisha ya mafanikio yanakuja kwa kuwajibika  na si kwa kulalamika au kuishi kwa lawama.

Waangalie kidogo watu ambao kila siku na kila wakati ni watu wa kuishi kwa lawama, mara nyingi watu hao hata pia kwenye maisha yao, hawapigi hatua sana. Hiyo ikiwa na maana kwamba lawama si nzuri katika kutafuta mafanikio.
Weka nguvu zako katika kuweka juhudi za kutafuta mafanikio na si kuweka juhudi zako katika kuwalaumu watu wengine kwamba hao ndio wameharibu maisha yako au mipango yako mizuri ambayo ulikuwa umejiwekea.
Kitu cha kufanya kwako wewe ni kuendelea kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kitu kipi kwamba ukirekebishe na kikusaidie kuweza kusonga mbele zaidi hapa kama ni kazi ni lazima ujue namna ya kufanya kazi yako kwa upya kabisa.
Usikubali kuchukua hatua kwa kutumia mdomo wako, usikubali kuchukua hatua kupitia maneno yako, amua kuwajibika juu ya maisha yako kwa kuchukua hatua za kubadili maisha yako na si kwa kulaumu ambako unakufanya.
Nikiwambie tu ukweli huu, hutaweza kufika popote kwenye maisha yako ya mafanikio kama kila siku utaendelea kulaumu wengine juu ya udhaifu wao na wewe kusahau udhaifu wako ulionao, hilo unatakiwa kulielewa.
Kitu cha kuelewa hapa ni kwamba, usipoteze muda na nguvu zako sana katika kulaumu, badala yake wekeza nguvu zako hizo katika swala zima la kuwajibika na hapo utakuwa na nafasi ya kujenga mafanikio yako sana.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.