google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 7, 2018

Kama Utashindwa Kufanya Kitu Hiki Kwanza, Acha Kuchukua Hatua.

No comments :
Tunajua wote ili kufikia mafanikio yako, ni lazima kwako wewe kuchukua hatua. Kusoma peke yake au kujifunza huko kote bado hakutoshi, bali hatua ni kitu cha muhimu sana ili uweze kufikia zile ndoto zako uzitakazo.
Pamoja na hatua ni muhimu sana na ni kitu cha lazima kufikia ndoto zako, lakini kama utashindwa kujitoa kikamilifu kwa kile ambacho unakwenda kukifanya, ni bora usichukue hatua kabisa. Hatua zako lazima ziendane na kujitoa kwako kikamifu.
Kuchukua hatua huku ukiwa unajua hujajitoa kikamilifu kutimiza ndoto zako hiyo itakuwa ni sawa na kazi bure na pia ni kupoteza muda wako. Ni bora ukajipanga na kujua kabisa jinsi utakavyojitoa kuliko kuchukua hatua pasipo kujitoa kikamilifu.
Ninasema hivyo kwa sababu moja kubwa, ukikutana na upinzani au changamoto kwa sababu hujajitoa kikamilifu hutaweza kuendelea tena ni lazima utasimama. Kule kusimama kwako kutakuja kwa sababu hujajitoa tu na si vinginevyo.

Hiyo yote inakuja kwako hivyo kwa sababu kile unachokifanya unakua hujajitoa kikamilifu kwa hiyo inakuwa ni sawa kabisa na kupoteza nguvu zako kwa makusudi ambazo ulikuwa umeziandaa ziweze kukusaidia kufikia ndoto zako.
Kila wakati unatakiwa kuweka kwenye akili na kujiuliza kwamba je, umeamua kufanya hicho unachotaka kukifanya?  je, umeamua kuchukua hatua? kama umuamua kuchukua hatua na kufanya, kitu unachotakiwa kukizingatia ni kujitoa na kuhakikisha hilo linatimia.
Acha mchezo wa kitoto wa kuamua kuchukua hatua za kukupeleka kwenye ndoto yako huku ukiwa hujajitoa kikamilifu. Kitu kitakachokufanikisha ni kwa wewe kuweza kujitoa kwako kwa ukamilifu na kukubali kukabiliana na kila aina ya changamoto inayojitokeza.
Kujitoa kwako ni ishara tosha inayoonyesha ni kweli unayataka mafanikio hayo. Hutakiwi kufanya kitu unachokwenda kukifanya kwa lelemama, unatakiwa kujitoa haswa ili kuweza kutimiza kile ulichoamua.
Ndio maana kabla hujachukua maamuzi ya kufanya kile unachotaka kukifanya, unatakiwa ujue uwe tayari kujitoa, ukishajua uko tayari kujitoa fanya kitu hicho ambacho unataka kukifanya na utaweza kufanikiwa.
Wapo watu ambao wanashindwa katika maisha kwa sababu ya kuamua kufanya mambo huku wakiwa hawajajitoa. Nafikiri watu hawa unawajua na pia inaweza ikawa wewe mwenyewe yaani unafanya jambo huku hujajitoa.
Matokeo ya kufanya jambo huku ukiwa hujajitoa itakupelekea sana wewe kufanya jambo lako kwa kulipua na hutafanya kwa ubora na ikiwa pamoja na kushindwa kwenye jambo hilo lazima kujitokeze, hutaweza kukwepa kushindwa kwa sababu hujajitoa kikamilifu.
Ni jambo la hatari sana kuchukua hatua huku unajua hujajitoa kikamilifu. Elewa hivi, kama unaona hauko tayari kujitoa kikamilifu kwa kile unachokifanya kama nilivyo kwambia ni bora usichukue hatua kabisa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.