google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 8, 2018

Mafanikio Ya kweli Yanapatikana Hivi…

No comments :

Hapo ulipo najua unatafuta mafanikio ya aina fulani, lakini je ulishajiuliza mafanikio hayo ukishayapata yatakuwa na msaada gani kwa wengine? Je, ni mafanikio ambayo ukiyapata yatakuwa ya ubinafsi au yatakuwa ni baraka kwa wengine.
Hili ni jambo la kawaida tu, lakini unapaswa kujiuliza na kulitilia maanani ili kujua mafanikio yako unayoyatafuta unataka yawe msaada kwa wengine au unataka yaweje? Ni wengi hawajiulizi jambo hili.
Lakini kwa jinsi ilivyo, ili mafanikio yako yawe ya maana na yaweze kukusaidia sana wewe, ni lazima mafanikio hayo yalete mabadiliko kwenye maisha ya wengine pia. Kwa jinsi mafanikio yako yanakuwa msaada kwa wengine, na wewe kufanikiwa kwako kunakua zaidi.
Hapa nikiwa na maana kwamba kufanikiwa kwako wewe kuwasaidie na wengine kuweza kupiga hatua za kimaisha. Hapa tena nikiwa na maana kwamba mafanikio yako wewe yaweze kuleta mabadikio chanya kwa jamii.

Kama unasema una mafanikio lakini wakati huo huo tukiangalia mafanikio hayo yanakufaidisha wewe tu na hakuna msaada kwa wengine naweza nikasema hayo mafanikio yanaweza kuwa ni batili.
Mafanikio ya kweli yanaleta mabadiliko katika jamii na kuifanya jamii inayokuzunguka ifaidi. Ukumbuke hapa simaanishi ugawe vitu hovyo au utoe msaada tu kila wakati, namaanisha hakikisha mafaniko yako yawe ya msaada kwa wengine, hata kwa kuwasaidia watu pia kutimiza malengo yao.
Ikiwa utalenga sana kutafuta mafanikio kwa ajili yako tu na si kwa ajili ya wengine pia, uwe na uhakika kuna wakati utafika utakutana na upinzani na hakuna mtu ambaye ataweza kuja kukusaidia kwa sababu ya ubinafsi wako.
Unapokuwa lakini unatafuta mafanikio huku akili yako imelenga kutafuta mafanikio ya ziada na ambayo yatawasaidia na watu wengine pia kuweza kupiga hatua, basi fursa nyingi zitafunguka  kwa sababu ya kile unachokidhamiria akilini mwako.
Hivi ndivyo naweza kusema mafanikio ya kweli yanapatikana, yaani yanapatikana kwa kuwa msaada kwa wengine. Huhitaji tu kuwa mbinafsi kwa kila kitu, hakikisha msaada wako kwa wengine unaonekana.
Ifanye jamii inayokuzunguka au watu wanaokuzunguka wajivunie mafanikio yako. Kuwa na falsafa ya kwamba 'nikifanikiwa mimi, na wengine wamefanikiwa na pia kushindwa kwangu mimi kuna wakawamisha na wengine pia.'
Ukiwaangaliwa watu wenye mafanikio makubwa ni watu ambao mafanikio yao pia yanawanufaisha na watu wanaowazunguka. Jaribu hata wewe kuchunguza kidogo hili utaliona kwa jinsi lilivyo.
Ukiona mtu anatafuta mafanikio lakini wakati huohuo ni mbinafsi sana, basi naweza kusema mafanikio yake yana shaka kubwa ndani mwake. Watu wenye mafanikio ya kweli, dalili ya kwanza ya mafanikio hayo ni kuwa msaada kwa wengine.
Najua hapo ulipo umefanikiwa kwa kiasi fulani, sasa je, mafanikio uliyonayo ni msaada na baraka kwa wengine? Sitaki unipe jibu lakini ukweli unaujua wewe. Weka jitihada za kutafuta mafanikio ya kweli kwa kuwa msaada wa wengine na utafika mbali.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,










No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.