google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 5, 2018

Maisha Uliyonayo Yako Hivyo Kwa Sababu Hii Kubwa.

No comments :
Jiangalie hapo ulipo, jiangalie nini ulichonacho na nini ambacho huna, ukijiangalia hapo ulipo na hali uliyonayo, basi ni matokeo ya kitu kimoja tu, ambacho si kingine bali vipaumbele ambavyo uliviweka wakati wa nyuma.
Vile vipaumbele ambavyo ulikuwa umeviweka kwenye maisha yako kwa siku za nyuma, hivyo ndivyo vimekufikisha hapo ulipo mpaka sasa. Ukiangalia mambo uliyokuwa ukiyazingatia, ndio yamekupa matokeo hayo.
Hakuna ambacho umekipata kwa bahati mbaya, kila kitu umekipata kwa sababu ya vipaumbele vyako. Huhitaji kubisha au kushangaa ni kitendo cha wewe kuchunguza kidogo tu na utagundua ni kweli vipaumbele vyako ndivyo vilikufikisha hapo.
Kwa hiyo uwe una hali mbaya kiuchumi, au uwe na maisha yeyote yale uliyonayo. Maisha hayo yametengenezwa na kitu kimoja tu ambacho ni vipaumbele vyako na sio kitu kingine chochote kile ambacho pengine unakifikiri.

Kama unajiona una maisha magumu na huridhiki nayo hata kidogo, kitu cha kwanza cha kuanza nacho ni kwa wewe kukazana kubadili vipaumbele vyako. Unapokazana kubadili vipaumbele vyako ndipo unatengeza mafanikio yako hapo.
Inawezekana vipaumbele ulivyokuwa navyo, ndivyo vimekufanya ukawa na maisha magumu sana. Sasa tatizo la watu wengi hawajui kufatilia vipaumbele vya maisha yao na wanaona maisha yao magumu tu pasipo hata kuelewa chanzo ni nini.
Jikague mwenyewe na ujiangalie vipaumbele vyako viko sahihi? Kama unaona vipaumbele vyako viko sahihi, basi kazana sana kufatilia vipaumbele hivyo mpaka viweze kukusaidia kuweza kufanikiwa na kufika mbali kimafanikio.
Watu wengi ukiangalia maisha yao yanakwama kwa sababu ni watu ambao wana vipaumbele ambavyo haviwasaidii kuweza kufikia ndoto zao za kimafanikio hata kidogo. Kwa kifupi vipaumbele vyao vinawadondosha.
Hakikisha vipaumbe ambavyo unajiwekea vinakwenda kubadilisha maisha yako na maisha yako sio lazima yabadilike sasa hivi ghafla, ni kwa kidogo kidogo itafika muda maisha yako yataweza kubadilika na kuwa bora zaidi.
Unatakiwa kujiuliza kila wakati je, vipaumbele vyangu hivi vinanisaidia kufikia mafanikio yangu? Au vipaumbele vyangu hivi havieleweki? Ukijua hivyo tafuta vipaumbele ambavyo viko sahihi na vyenye manufaa kwako.
Usikubali kuwa miongoni mwa watu ambao wanaharibu maisha yao kwa sababu ya kukosa vipaumbele vya msingi. Kuwa miongoni mwa watu ambao watatengeneza maisha ya mafanikio kwa sababu ya kujenga vipaumbele sahihi.
Nikutakie siku njema na wakati mwema katika kutekeleza vipaumbele vyako ili vikusaidie kufikia malengo yako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.