google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 22, 2018

Kama Utachagua Njia Hii Ya Mafanikio, Hutaweza Kufanikiwa.

No comments :
Hakuna kitu rahisi kama kutokuamua kufanya kitu. Kusema inaweza ikawa rahisi kwamba nitafanya jambo hili, lakini kuchukua hatua inakuwa ngumu, hiyo yote inaonyesha kutokufanya kitu ni jambo rahisi sana ambalo kila mtu analiweza.
Mara nyingi pia mambo rahisi hayawezi kukupa kitu bora. Kila unachotaka kukifanya ukigundua kwamba kitu hicho ni rahisi na kinafanywa na kila mtu, ujue kabisa kitu hicho si rahisi sana pia kutoa matokeo yale yaliyo bora.
Ni rahisi sana kuwa na matumaini ya matokeo bora kwa kile unachokifanya, lakini uelewe kabisa ili hayo matokeo uweze kuyapata unahitajika kwanza kuweka juhudi na kufanya kazi kweli na si kutegemea rahisi.

Ukiona una mawazo ya kupata mafanikio kwa urahisi sana, kila kitu unakitaka kwa urahisi na unaamini hivyo kabisa, ujue kabisa kushindwa hutaweza kukwepa. Ili kufanikiwa inatakiwa juhudi na si swala la urahisi kama unavyowaza.
Ni rahisi sana kuwakosoa watu wengine kwa yale mambo wanayoyafanya, na ukijiangalia wewe hufanyi kitu na mbaya zaidi huwezi kufanikisha jambo lolote lile kwa kuwakosoa watu wengine wanaochukua hatua.
Ukitaka upige hatua za kimafanikio, huhitaji kuwa mtu wa kukosoa sana wengine. Ukiona unaanza kuwakosoa na wakati wewe huchukui hatua, unatakiwa kukaa kimya tu, kwani hakuna unachokifanya na unataka kufanya rahisi tu kukosoa ambako si msaada kwako.
Mafanikio ya kweli yanakuja na wale watu ambao kweli wameamua kuchukua hatua na si kuwa wakaaji ambao hawachukui hatua ila kazi ni kukosoa. Nikwambie tu unaweza ukawakosoa wengi, lakini yote hiyo haikusaidii kitu, unatakiwa kuchukua hatua.
Ikiwa unataka kweli kufanikiwa unatakiwa kufuata na njia ngumu, njia ambayo si rahisi lakini ambayo mwisho wa siku itakufanikisha. Kuchukua njia rahisi au kuamua kufanya mambo rahisi rahisi ujue kabisa huko ndiko unapotea kimafanikio.
Fanya maamuzi ya kutokuchagua njia rahisi ya mafanikio yako. Njia rahisi ya mafanikio haina msaada na haiwezi kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa. Wengi wanapitia njia hii na wanaishia kukwama sana na kutokuweza kufanikia kabisa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.