google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 30, 2018

Jikumbushe Kila Mara Mambo Haya Ili Yakupe Hamasa Ya Kufanikiwa.

No comments :
Najua hapo ulipo, kwa chochote kile unachokifanya, lengo lako kubwa ni kuhitaji maisha mazuri na bora. Kuna maisha ambayo najua unayatamani, maisha hayo unataka kuyafikia na pengine una kiu nayo  sana.
Hata hivyo kabla hujafikia mahali ukayatamani sana maisha hayo unayoyataka, hebu jiulize, kwa jinsi maisha yako unavyoyaendesha na kwa jinsi unavyoendesha maisha yako kwa kila siku je, jinsi hiyo inakurushu kuyapata maisha hayo?
Ni wajibu wako kujikagau na kujiangalia wewe mwenyewe hatua kwa hatua kwa jinsi unavyoishi maisha yako. Kama kuna kitu unaona hakijakaa sawa na unaendelea nacho ujue kitu hicho kitakunyima kuweza kufanikiwa.
Mwenendo wa wewe jinsi unavyoishi siku moja tu, unaweza ukatoa picha kamili ya kwamba unafanikiwa au hufanikiwi bila kujali ni kitu gani ambacho unakifanya. Mara nyingi nasema kwenye kufanikiwa hakuna uchawi ni kanuni na sheria tu.
Unaweza ukajiuliza mwenyewe kama kweli unataka mafanikio hasa, je, ni kweli mafanikio hayo utayapata kwa jinsi unavyopoteza muda hovyo. Jiulize wewe mwenyewe na usimwambie mtu yeyote, lakini ujipe majibu sahihi pia.

Tena jiulize, kama unataka mafanikio ni kweli mafanikio hayo utayapa kwa wewe kuendelea kuwa mzembe na wala huweki juhudi zinazotakiwa? Je, ni rahisi kuyapata mafanikio hayo ambayo unayataka?
Na tena jiulize ama kweli unataka mafanikio, je mafanikio hayo utayapa kwa mwendo huo ambao unao ambao unaishi kiholela na hutaki kujifunza mambo mapya na hata kujichanganya na watu wengine?
Ongeza tena swali lingine hapo, kama unataka kweli mafanikio, je, mafanikio hayo utayapata kweli kwa jinsi unavyotapanya pesa zako huko na huko na kushindwa hata kujiwekea akiba ambayo itakusaidia?
Hutakiwi haya maswali ujiulize huku watu wengine wakisikia, unatakiwa kujiuliza wewe na kuangalia kule unakokwenda na pale ulipo ni nini unachokifanya, hatua zipi unazozichukua na zinakupeleka kwenya mafanikio au la.
Ili kufafanikiwa na kufikia mafanikio siku zote unatakiwa sana wewe kuwa makini kwa kila hatua. Unatakiwa kuwa makini kwa kuangalia mwenendo wako. Watu wengi wanapotea kwenye safari ya mafanikio kwa sababu si watu makini na wanakuwa wapo wapo tu.
Amua kuwa ‘siriazi’ kufatuta mafanikio yako na kuamua kuachana na kila aina ya uzembe ambao umekuwa ukikukwamisha hata wakati mwingine pasipo wewe kuweza kujua. Tupilia mbali uzembe huo na jikumbushe misingi ya mafanikio jinsi ilivyo.
Kila hatua unayoipiga,ujue kabisa ni kitu gani ambacho unakifanya, kuwa makini na kila hatua, hiyo itakuwa ni njia bora na ya pekee sana kuweza kukusaidia kuweza kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa uyatakao.
Ukipoteza umakini kwenye maisha yako na ukasahau kujikumbusha mambo ya kukusaidia kufanikiwa, basi hicho ni chanzo kikubwa sana cha wewe kuweza kuanza kupotea na kushindwa kuweza kufanikiwa. Unataka kufanikiwa usipoteze umakini.
Usikubali kushindwa, usikubali kupoteza maisha yako ya mafanikio eti kwa sababu ya kuendesha maisha yako kiholela. Kuwa makini na kila kinachokuzunguka katika kuhakikisha unafikia mafanikio pasipo kizuizi kikubwa sana.
Kila wakati jenga utaratibu wa kujikumbusha na kuangalia jinsi unavyoishi, je, kwa mwendo huo unaoishi, utakupa mafanikio au hautakupa mafanikio zaidi ya kuweza kukuangusha wewe mwenyewe?

Fanyia kazi hiki ulichojifunza leo kwa kuhakikisha kwamba, unajikumbusha yale maisha unayoishi au matendo unayoyafanya kama matendo hayo yanakusaidia kukupeleka kwenye mafanikio uyatakayo au yanakupeleka kwenye kushindwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.