google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 23, 2018

Usijidanganye, Hutaweza Kufanikiwa Kama Utakuwa Una Malengo Haya.

No comments :
Ikiwa leo utakwenda kwa daktari na kumwambia kwamba unaumwa na kisha ukaamua kuisha hapo bila kuendelea kueleza zaidi ya unaumwa nini, daktari kwa kawaida hata weza kukupa dawa zaidi itabidi akuulize nini shida yako zaidi.
Daktari huyu atafanya hivi kutaka kujua ugonjwa unaoumwa ni upi , na ugonjwa huo umeanza lini. Taarifa hizi ni muhimu sana kwa daktari kwa sababu, taarifa hizo ndizo zitakazoweza kumwongoza yeye ili aweze kukupa tiba sahihi.
Pia hata leo hii kama umeamua kusafiri kwa kutumia basi la abiria na ukaenda kwa wakatisha tiketi ukamwambia nataka kusafiri, ujue kabisa wauza tiketi za safari hawawezi kukupa tiketi au kukuuzia mpaka uulizwe unataka kusafiri kwenda wapi.
Pia muuza tiketi taarifa hizi za wewe unaenda wapi zinakuwa ni muhimu sana kwake ili aweze kukupa gari sahihi ambayo inaenda kule unakotaka, kinyume cha hapo asipofanya hivyo atakupoteza na usifike kule unakotaka kwenda kwenye safari yako.

Na katika maisha ya mafanikio  mambo yako hivyo hivyo. Kama unataka kufanikiwa kuwa na mawazo mazuri peke yake hiyo haitoshi na kusema kwamba hapo ndio lazima utafanikiwa kwa sababu una mawazo mazuri.
Pia hata kule tu kusema kwamba nataka kufanikiwa haitoshi, unatakiwa uwe na mawazo ya kujua unataka kufika wapi yaani uwe na wazo maalumu ya kuelewa kwa ufasaha ni kitu kipi unachokitaka kwenye maisha yako.
Unatakiwa ujue unataka kufanikiwa katika eneo lipi, nini ambacho utakwenda kufanya kila siku ili kiweze kukusaidia kufanikiwa katika hicho ambacho unataka kufanikiwa nacho. Kwa hiyo hapa unaona ni lazima uwe na mawazo maalumu na yenye mwelekeo maalumu.
Kama tulivyoona hata kama unaumwa vipi, huwezi kupona kwa kusema kwamba naumwa nahitaji dawa, hutapona kwa sababu daktari hata jua unaumwa nini na ni dawa gani, kwa hiyo ni lazima ueleze unaumwa nini, na mafanikio yako hivyo.
Muujiza wa mafanikio yako utaanza kuonekana wakati ambapo utakuwa unajua ni nini unachokitaka, mwelekeo wako ni upi na unataka kufanikiwa kwa kufanya kitu kipi yaani utafanikiwa kwa wewe kuwa ‘specific’ kwa kile ukifanyacho.
Usijidanganye, hutaweza kufanikiwa kama utakuwa una malengo ya jumla ya kusema nataka kufanikiwa. Utafanikiwa kwa kuwa na malengo maalumu ya kujua vizuri kile ambacho unataka kikufanikishe ni kitu kipi hasa.
Acha kuchelewa, anza leo kuwa na malengo maalumu, usiwe na malengo ya jumla ya kusema nataka kufanikiwa. Ifike mahali ujue ni nini unachokitaka ili ufanikiwe na hayo mafanikio yako kwa makadirio utayataka baada ya muda upi.
Ila kitendo cha kuwa tu na mawazo ya jumla ya kimafanikio huko ni sawa na kuamua  kujidanganya, lakini ukweli wa wazi ni kwamba hata ufanyaje hutaweza kufanikiwa kama utakuwa na malengo ya jumla ya kimafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.