google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 26, 2018

Ukimudu Kufanya Jambo Hili Kwa Uhakika Na Mengine Mengi Utayaweza.

No comments :
Unapopata kitu kizuri iwe ni mafanikio au kitu chochote kile, kitu hicho ni rahisi kuweza kukusaidia kuendelea kupata mambo mengine mazuri zaidi kwenye maisha yako. Hiyo ikiwa na maana mambo mazuri yanaweza kukuongoza kupata mambo mengine mazuri pia.
Kuboresha eneo moja la maisha yako kwa uhakika inakusaidia sana kuweza kuboresha maeneo mengine. Kama hujui ni wapi unatakiwa kuanzia, anzia hapo ulipo na kwa chochote kile unachokifanya kwenye maisha.
Anza leo kuwekeza kidogo, ukifanikiwa kuwekeza kwa hicho kidogo itakusaidia sana kuweza kuwekeza kwa makubwa. Ni muhimu kujua kufanikiwa kwa jambo moja ni rahisi kufanikiwa kwa mengine pia.
Ndio maana kila wakati unatakiwa ujue namna ya kuweza kuthubu. Kama wewe ni mtu wa kuthubu maanake unataka kufanikiwa na kufanikiwa kwako huko ndiko ambako kunakokupelekea ufanikiwe kwa mambo mengi zaidi.

Huwezi kupiga hatua kubwa au kama kila kitu hufanikishi. Unatakiwa kufanikisha mpango wako hatakama ni kidogo sana, kwani kwa kufanikiwa huko hiyo inakuongoza kuweza kufikia mafanikio makubwa.
Ninachotaka kusema hapa  ni kwamba, ushindi mdogo ni hatua nzuri sana kwako ya kukusaidia kuweza kupata ushindi mkubwa. Kwa jinsi unavyopata mshindi mdogo unakusaidia kukupa kujiamini na kusababisha kutenda makubwa zaidi ya hayo.
Unatakiwa sasa kuzingatia kwa chochote kile ukifanyacho unatakiwa ukifanye kwa ushindi. Kwa jinsi unavyopata ushindi mwingi mdogo mdogo na ushindi huo unakusaidia kukupa mafanikio makubwa uyatakayo maishani mwako.
Ikiwa unataka kuwa miongoni mwa watu wenye mafanikio duniani, chukua hatua ya kufanya hata kama kitu kidogo ila iwe kwa ushindi. Kama nilivyosema kwa ushindi huo mdogo utakuwezesha kushinda na kupata ushindi mkubwa pia.
Ndio maana nakwambia ukimudu kuweza kupata ushindi mdogo kila wakati, sina wasi wasi na ushindi mkubwa utakuwa ni rahisi kuupata hivyo hivyo kwako. Anza kushinda vitu vidogo vidogo kwanza kwenye maisha yako ili vikusaidie kushinda makubwa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.