google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 14, 2018

Kufanikiwa Au Kushindwa Kunatengenezwa Sana Na Mambo Haya…

No comments :
Mafanikio utayapata , kama utadhamiria kweli kuifanya dunia kuwa sehemu bora kuliko sasa, na kushindwa kutakuja kwako kama wewe utaiona dunia ni sehemu mbaya na tena iko kinyume na wewe, kwa hiyo hapa ni lazima utaweza kushindwa.
Mafanikio yatakuja kwenye maisha yako kama utakuwa mtu wa kutafuta na kutengeneza thamani. Kushindwa kunakuja kwenye maisha yako, kama unategemea dunia itakupa kitu na utaishi kwa thamani zilizotengenezwa na watu wengine.
Mafanikio yatakuja kwenye maisha yako kama utafungua milango ya kujifunza zaidi kutoka kwa wengine na kwenye vitabu. Kushindwa kutaanza kukunyemelea hasa pale inapofika wakati ukasema kwamba wewe unaweza kila kitu.

Mafanikio yatakuja kwako, ikiwa utakuwa mtu wa kutazama chanya na kuangalia fursa zinazokuzunguka. Kushindwa kutakuja kwako ikiwa tu, utakuwa mtu wa kutoa sababu kila wakati na kushindwa kuangalia mambo ya kukusaidia.
Mafanikio ni matokeo ya mawazo, mtazamo wako na juhudi unazoziweka kila siku katika kuweza kufikia mafanikio. Na kushindwa pia ni matokeo ya mawazo, mtazamo na juhudi zako. Iwe kushinda au kushindwa kunatokana sana na mambo hayo matatu.
Ukiona mtu yeyote amefanikiwa maeneo matatu ambayo yana mchango mkubwa sana wa kushindwa au kufanikiwa kwake ni hayo. Unachotakiwa kufanya ni kuyatumia maeneo hayo ambayo ni mawazo, mtazamo na juhudi kwa vizuri.
Unaweza ukajikuta kila mara unashindwa sana kwenye maisha yako kwa sababu ya kushindwa kutumia mawazo yako vizuri. Unatakiwa kutumia mawazo yako kwa uhakika kufikiri fursa na mambo ya kukusaidia kufanikiwa.
Pia unaweza kila wakati ukiwa unashindwa kwa sababu ya kuwa na mtazamo ambao sio sahihi. Kile ambacho wenzako wanaona kinawasaidia wewe huoni. Unapokuwa na mtazamo kama huu ambao ni duni, kufanikiwa kwako kutakuwa ni shida sana.
Unaweza pia ukajikuta ni mtu wa kushindwa, kwa sababu ya juhudi zako hazitoshelezi kufika kule kwenye mafanikio sahihi. Unatakiwa uweke juhudi sahihi na kwa nguvu zote katika kutengeneza mafanikio yako.
Ili kufanikiwa unapaswa kujua na kulewa, mafanikio yako yanatengenezwa sana mambo haya matatu ambayo ni mawazo, mtazamo na juhudi zako. Yafanyie kazi mambo haya matatu na kisha utaona matokeo yake.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.