google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 28, 2018

Usipoliangalia Jambo Hili Kwa Umakini Litakufanya Ushindwe Kufanikiwa.

No comments :

Kati ya kitu kimojawapo ambacho kitakupelekea wewe kuanguka kwenye maisha yako kama usipokiangalia vizuri na kukijua jinsi ya kukabiliana nacho, ni kukatishwa tamaa. Usipokuwa makini na kukatishwa tamaa kwa namna yoyote ile lazima ukwame.
Maisha ya watu wengi yameishia kati na yamekuwa maisha ya ndoto na yale matumaini makubwa waliyokuwa nao watu hao mwanzoni yamepotea kabisa, yote hiyo ni kwa sababu ya kukatishwa tamaa iwe na wengine au wao wenyewe.
Inapifika mahali kwenye maisha yako ukaona kabisa kwamba wewe ndio umekata tamaa, naomba nikwambie kwamba wewe ndio basi tena kufanikiwa. Hutaweza kufanikiwa mpaka urudi kwenye matumaini ya kuamini kwamba utafanikiwa tena.
Kukatishwa tamaa kwa namna yoyote ile kunakupotezea sana nguvu zako ambazo ulikuwa umejiandaa nazo kwa ajili ya kuchukua hatua. Kwa bahati mbaya kukatishwa tamaa kwenyewe kunaweza kukawa kwa maneno tu, ambayo umeyasikia na hayana ukweli.

Ndipo hapo ambapo unatakiwa ujiulize ni kwa jinsi gani maneno hayo yana nguvu au yana ukweli na ule uhalisia. Kama una nia kweli ya kufanikiwa unayo, inatakiwa uzibe masikio kabisa na usisikie kukatishwa tamaa kwa namna yoyote kukitokea kwako au kwa wengine.
Ili uwe mshindi wa mafanikio hutakiwi kuwa mtu wa kukata tamaa. Unatakiwa uwe mtu ambaye una roho ngumu, lakini si roho ya kuwakomoa watu, bali ile roho ya kuamua kutokatishwa tamaa na kitu chochote kile zaidi ya kutaka kuona ukifanikiwa.
Unapaswa kuelewa, juhudi yoyote kwenye maisha yako iwe juhudi ya masomo, juhudi ya kutaka kufikia mradi fulani au juhudi ya aina yoyote ambayo lengo lake ni kukufanikisha, juhudi hiyo ni lazima huwa inakutana na kukatishwa na tamaa.
Utakuta juhudi zako zinakatishwa tamaa na mazingira na kufika mahali unaona duu hakuna kinachofanikiwa tena hapa. Pia wakati mwingine utakuta juhudi zako zinakatishwa tamaa na wewe mwenyewe kutokana na mawazo yako au wale wote wanaokuzunguka.
Kitu cha namna hii kinapokutokea si bahati mbaya, bali naweza nikasema kwamba unatakiwa ujue juhudi yoyote ile kwa namna moja au nyingine upo muda wake utafika inakuwa inatishwa tamaa na vitu vingi sana na kama usipokuwa makini utakwama.
Hata hivyo unachotakiwa kuelewa hapa, huwezi kukwepa kwenye maisha yako kukatishwa tamaa kwa namna yoyote ile. Kitu pekee ambacho unaweza kukifanya hasa pale unapokatishwa tamaa je, unachukuliaje kukatishwa tamaa huko?
Fanya kukatishwa tamaa kwako iwe sababu ya kujitoa zaidi mpaka kuona ndoto zako zinatimia. Usikubali kuachia ndoto zako kirahisi eti kwa sababu umekatishwa tamaa. Tumia kukatishwa tamaa kokote kule kunakokutokea kwako kwa faida.
Ukiwa mwangalifu na ukajua jinsi ya kukabiliana na kukatishwa na tamaa, utaweza kuzifikia ndoto zako, lakini usipojua vizuri jinsi ya kukabiliana na kukatishwa tamaa, jambo hili litakusumbua sana na utashindwa kwenye maisha yako.
Je, kukatishwa tamaa kwako unakuchukuliaje kwenye maisha yako, ni chanzo cha kufanikiwa au kushindwa kabisa? Usisite kutoa maoni yako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.