google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 24, 2018

Kitu Ambacho Hutakiwi Kukisahau Wakati Unayatafuta Mafanikio.

No comments :
Mafanikio yanawatenga watu wengi sana, kulingana na watu hao jinsi wanavyoyachukulia mafanikio yenyewe. Ukiangalia wengi wanayachukulia sana mafanikio kama pesa au umaarufu kwamba hayo ndiyo mafanikio halisi.
Ikiwa utakuwa unayaangalia mafanikio tu kwa jicho la kuangalia vitu vya nje, basi utakuwa unapishana sana na mafanikio yako. Hutakiwi kutazama mafanikio kwa jicho moja, unatakiwa kuyatazama mafanikio bila kusahau kitu kimoja muhimu sana ambacho nakwenda kukueleza.
Kitu ambacho hutakiwi kukisahau wakati unayatafuta mafanikio au wakati unayatafsiri mafanikio kwa jinsi unavyojua wewe ni kwamba mafanikio yanaletwa na thamani. Hata uwe unatafuta mafanikio ya aina gani kwanza lazima uanze na kutoa thamani.

Kama unajua mafanikio yanaletwa na thamani, basi kazana kutoa thamani sana. Na kila unapotoa thamani, hata kwa nje kama sisi hatuoni mabadiliko makubwa lakini hayo ndiyo mafanikio yenyewe na mafanikio ya nje itafika wakati yataonekana tu.
Unachotakiwa kujiuliza kila wakati ni kwamba kitu gani ambacho unatakiwa kukikamilisha na hujakikamilisha? Ukishakiona kitu hicho toa thamani zaidi ili kikupe mafanikio. Kila  wakati kazana kutoa thamani na utaishi maisha  sawa na tajiri yeyote yule duniani.
Huhitaji pesa, huhitaji umaarufu au nguvu yoyote kubwa ili uweze kufanikiwa, unachohitaji wewe ni kuweka thamani. Ukikazana na kuweka thamani na ukaipa dunia kile inachotaka, itafika  mahali utalipwa tu na hakuna kitakachoshindikana kwako.
Kwa hiyo badala ya kuanza kufikiria pesa utakazopata kwanza, badala ya kuanza kufikiria utajiri kwanza utakaoupata, anza kujizoesha kufikiria kwanza ni thamani ipi ambayo wewe utaitengenza na itakupa mafanikio.
Nasema hivyo kwa sababu pasipo kutoa thamani, hata hayo mafanikio uyatake vipi hutaweza kuyapata kwenye maisha yako zaidi utaishia kuyasikia kwenye redio au kwenye maisha ya wengine, lakini sio kwako.
Dunia kwa jinsi ilivyo inataka vitu vizuri, inataka kuona madiliko, dunia inatake kuonja radha tofauti, sasa hivyo vyote vinapatikana kwa kutoa kitu cha thamani. Huhitaji kusubiri kutoa thamani, anza kuweka juhudi wa kile unachokifanya sasa.
Katika mafanikio hakuna hali ya ukawaida. Unapoona una ukawaida wowote ule ujue hakuna thamani inayozalishwa hapo na mwisho wa siku utaishia kwenye kushindwa vibaya na hata usilaumu mtu yeyote yule.
Kila siku ni nafasi kwako wewe ya kuweza kutengeza thamani kubwa juu ya maisha yako. Usipoteze na wala usiendelee kusubiri thamani hiyo ikapotea. Weka juhudi za kuhakikisha unabadili maisha yako na ila kitu kitakaa sawa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,








No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.