google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 12, 2018

Kama Ukifanya Mambo Hayo Na Yasipokupa Mafanikio, Hutaweza Kufanikiwa Tena.

No comments :
Katika harakati za kutafuta mafanikio yapo mambo mengi sana ambayo unatakiwa uyajue ili yakusaidie kukua kimafanikio. Kutokujua mambo hayo ndiyo chanzo kikubwa cha watu wengi kuweza kushindwa katika maisha ya mafanikio.
Leo katika makala haya, sitaki kukwambia mambo yote hayo, nataka nikwambie mambo matatu tu, ambayo kama ukiyafanya na ukijipa muda wa kutosha ni lazima yatakupa matokeo ya kuweza kubadilisha maisha yako.
1. Anza na kidogo.
Ili kufanikiwa na kuweza kufanya mafanikio yako yakazidi kuonekana hata kama huna kitu,  unatakiwa kujifunza kuanza na kidogo ulichonacho. Si lazima kuanza na makubwa sana, anza na kile kidogo  ulichonacho.
Unapoanza na kidogo kitu ambacho hutakiwi kusahau ni kuweka nguvu zako zote hapo na kujituma kisawasawa hadi kuweza kufanikiwa. Hakuna mafanikio yanayoanza kwa mara moja na kuwa makubwa, mafanikio yote yanaanza kwa kidogo kidogo.
Kwa hiyo kama unafikiri mafanikio makubwa, usifikirie mara moja kufika tu kule unakotaka kufika, anzia kwanza pale ulipo na kisha utakuwa unakua taratibu kwa jinsi siku zinavyokwenda. Hutakiwi kuwa na haraka, anza na kidogo na uwe mvumilivu.
Hili ni jambo mojawapo muhimu sana kama ukilifanya na kweli ukaamua kuanza na kidogo, nakuhakikishia ni lazima utafanikiwa. Kikubwa usife moyo kwa kuanza kwako na kidogo, endelea kusonga mbele na utafanikiwa sana.

2. Endelea kufanya.
Inawezekana umejipa moyo na umekubali kuanza na kidogo, lakini nikwambie ukweli hata hivyo mambo hayataenda kwa urahisi kama unavyofikiri, huko njiani utakutana na changamoto na vizuizi vya kila aina ambavyo vitakukatisha tamaa sana.
Katika wakati ambao utakutana na changamoto, naomba nikwambie, huo si wakati wa wewe kuweza kukata tamaa au wakati wa wewe kuweza kusimama, endelea kusonga mbele, hapo ndipo siri ya mafanikio ilipo.
Ndio maana watu wenye mafanikio wanafanikiwa kwa sababu ya kukubali kuendelea kusonga mbele bila kujali wanakutana na changamoto za aina gani na ambazo zinawasumbua kwenye maisha yao.
Hata wewe usikubali kusimama, usikubali kutoa sababu, toa matokeo yatakayoweza kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa. Amua kuendelea mbele bila kujali una maisha ya aina gani mbele yako. ukiamua hivyo utafanikiwa nakwambia.
3. Wajibika.
Ni kweli umeamua kuanza na kidogo ulichonacho na pia umekubali kuendelea ingawa unakutana na changamoto, sasa usiishie hapo tu kubali kuwajibika kwa asilimia zote kwa hicho unachokifanya.
Badala ya kulaumu au kulalalamika, wewe weka juhudi, tengeneza thamani itakayozalisha mafanikio na weka nguvu zako zote za uzingativu kwa hicho unachokifanya ili uweze kupata mafanikio makubwa na ya uhakika.
Maisha yako hayawezi kubaki hapo yalipo, kama kweli umeamua kuwajibika, maana hautakubali kushindwa ni lazima utawajibika kupigania maisha yako mpaka yakupe mafanikio yale unayoyataka na itakuwa hivyo.
Wengi ukiangalia wanashindwa kwenye maisha kwa sababu hawakubali kuwajibika, kikitokea kitu kidogo tu juu ya maisha wanalalamika sana na kuona kila kitu basi kimeshindikana au kimeharibika.
Nikuhakikishie tu, kama huna kitu na ukifanya mambo haya kwa muda mrefu na yasipokupa mafanikio, hutaweza kufanikiwa tena. Haya ni ambayo ukiyafanya kwa kumaanisha yanazalisha matunda ya mafanikio yako.
Zingatia mambo haya, na yafanyie kazi ili kuhakikisha ndoto zako zinaweza kutimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.