google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 9, 2018

Kama Una Sifa Hii Muhimu...Itakupa Mafanikio Makubwa.

No comments :
Waangalie watu wanaopata matokeo na mafanikio makubwa kwa yale mambo wanayoyafanya. Kila ukiwaangalia watu hawa wana sifa moja kubwa inayofanana, na sifa hii si nyingine bali ni kujali sana kile wanachokifanya.
Hakuna mtu ambaye aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa akawa hajali kwa kiasi kikubwa kile ambacho anachokifanya. Watu hawa wanajali sana bila kujali wanachokifanya iwe ni huduma au biashara ambazo wanazimiliki. Sifa hii ni muhimu sana kwao.
Na kutokana na kujali huko hujikuta ni watu wa kujifunza makosa, na hatimaye kuweza kuboresha kazi zao ambazo inafika wakati ziwapa mafanikio makubwa sana ambayo kila mtu anayashangaa kwa nje, kumbe kila kitu kimeanzia na kujali.
Unatakiwa kuelewa, unapoamua kujali kile unachokifanya, bila kuangalia kitu hicho ni kidogo au kikubwa kiasi gani, kiasili wewe unakwenda kufanikiwa moja kwa moja. Hakuna namna mafanikio ambavyo yanaweza yakakutupa kama unajali ukifanyacho.

Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye maisha kwa sababu ya kushindwa kujali kile wanachokifanya. Utakuta mtu ni mfanyabiashara hajali sana kuhusu wateja na mambo ya msingi  yanayohusiana na biashara yake.
Pia utakuta mtu mwingine labda ni mwanariadha au mwana michezo wa aina fulani, lakini naye hajali huo mchezo wake kwa kiasi kikubwa. Ipo mifano mingi ambayo inaonyesha kwa watu wengine kutokujali, na hupelekea moja kwa moja anguko la mafanikio yao.
Unaweza ukajiangalia na kujitafakari wewe hapo ulipo,je, hicho unachokifanya unakijali kwa kiasi gani? Je, unakijali kiasi cha kwamba kitu hicho kinaweza kikakupa mafanikio makubwa uyatakayo leo na kesho?
Ili kujenga mafanikio makubwa, anza kujali kile unachokifanya. Kwa kujali kile unachokifanya itapelekea wewe kutoa thamani inayotakiwa kwa kitu hicho na hapo ndipo mafanikio yako yatakapoanza kuchipukia.
Unatakiwa kujali kile ambacho wewe unakifanya, kwani wewe ndie mtu pekee ambaye unaweza kujali na kuleta mabadiliko kwa kitu hicho. Ukumbuke usipojali kitu hicho hakuna mwingine ambaye anaweza akafanya hivyo kwa mbadala wako.
Tumia muda wako kufanya kile unachokifanya na huku ukijali kwa asilimia zote. Hivi ndivyo watu wenye mafanikio wanakuwa wanatofautiana na watu wa kawaida au watu wasio na mafanikio kwa kujali yale wanayoyafanya.
Ikiwa utajenga tabia ya kujali kile unachokifanya, utaanza kubadili hali ya kitu hicho na kuwa bora siku hadi siku. Na ubora wa kitu ukumbuke hayo ndiyo mafanikio, kila mtu anapenda kilicho bora na ukijali ukifanyacho utatengeneza ubora huo sana.
Usikubali hata siku moja kukaa upande wa kufanya jambo lako pasipo kujali. Ikiwa  kweli unaamua kukaa upande huo huo, nikwambie tu utakuwa wewe ndio umejitengenezea kushindwa kabisa kwenye kile ukifanyacho.
Chukua hatua leo, ya kuamua kufanya kile unachokifanya kwa kukijali kwa moyo wote. kwa kujali kitu hicho kama nilivyokwambia, ni chanzo cha kupata mafanikio yako kwani kitu hicho utakifanya kwa uhakika na kujifunza mambo mengi yatakayokubadilisha.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.