google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 15, 2018

Mambo Kumi (10) Unayopaswa Kuyazingatia Katika Safari Yako Ya Mafanikio.

No comments :
Yapo mambo ya msingi ambayo kila msaka mafanikio ni lazima ayafahamu katika safari yake ya mafanikio, na mambo hayo ya msingi yatamfanya mtu huyo aweze kuishi katika misingi hiyo ya mafanikio. Na mambo hayo ni:


1. Njia ya kuelekea kwenye mafanikio na njia ya kushindwa katika kufikia mafanikio  mara nyingi zinafanana, hivyo ni vyema kila wakati ukajifunza kuchagua njia sahihi ya kukupeleka kwenye mafanikio unayoyoyahitaji.

2. Mara zote ikumbukwe ya kwamba fursa zote unazoziona na usiziona huwa hazitokei kama ajali bali hutengenezwa hivyo jifunze kutengeneza fursa ili uweze kufikia katika kilele cha mafanikio yako.

3. Kutengeneza mafanikio  pekee yake haitoshi, bali jifunze pia kujitengenezea thamani kubwa katika jamii ambayo inakuzunguka, Thamani hii ina manufaa sana kwako na jamii inayokuzunguka.


4.     Kama hautakuwa tayari kupoteza au kupata hasara katika jambo lolote unalolifanya sahau kabisa kuhusu mafanikio.

5. Kila wakati naomba utambue ya kwamba mafanikio hujengwa na msingi kwa kutoka katika mazoea uliyoyazoea.

6.  Mara zote achana na tabia ya kuzungumza sana kuhusu malengo yako, bali unatakiwa kuyaweka malengo hayo  katika vitendo.

7.  Hakuna siri za mafanikio isipokuwa na maandalizi thabiti ya mafanikio hayo, kufanya kazi kwa bidii na kujifunza kutokana na makosa unayopitia.

8. Kama kweli unataka mafanikio na ili ufikie mafanikio hayo tambua unatakiwa kutokuwa mtu wa visinginzio hivyo epuka visingizio kila wakati.

9. Mafanikio sio ufunguo wa furaha bali furaha ndiyo ufunguo wa mafanikio, hivyo ili uweze kuitengeneza furaha hiyo unatakiwa kupenda hasa kile unachokifanya.

10. Kushindwa katika jambo unalolifanya isiwe kigezo ya kwamba huwezi kufanikiwa, bali unaposhindwa  kama jambo fulani ndiyo fursa pia mara zote kumbuka kuanguka mara nane ni fursa ya kuinuka mara tisa.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada cha msingi ni kuyazingatia hayo ambayo nimekueleza siku ya leo. Nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Ndimi Afisa Mipango, Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com
0757-909942

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.