google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 19, 2018

Hufanikiwi Sana Kwenye Maisha Yako, Kwa Sababu Bado Hujui Kitu Hiki Kilipo.

No comments :
Kuna eneo fulani katika maisha yako ipo hazina yako ya mafanikio, ambapo hazina hiyo wewe kwa sasa huijui ilipo, lakini hazina hii ilipo hapo ndipo kwenye mafanikio yako na hazina hiyo inakusubiria wewe uweze kuifikia na kuifanyia kazi.
Mahala ilipo hazina yako ni eneo ambalo unatakiwa uligundue, lakini kwa bahati mbaya mpaka sasa hujagundua hazina hiyo ilipo. Mahali ambapo hazina yako ipo ni eneo ambalo unatakiwa kulifanyia kazi sana na uchunguzi mkubwa ili kulibaini.
Kitu ambacho nataka nikuulize wewe,  je, unajua eneo ambalo ipo hazina yako mpaka sasa? Je, unajua ni wapi ambako unaweza ukaipata hazina yako na hazina hiyo ya thamani utakuwa umeipata baada ya muda gani?
Inawezekana hazina yako imejificha sana kwenye maarifa, ambapo inakutaka wewe kutumia muda na kuyatumia maarifa hayo ili yakufanikishe. Kinachotokea hazina hiyo huifikii kwa sasa ni kwa sababu hujafika kiwango cha juu kutumia maarifa hayo.
Pia inawezekana hazina yako imejificha kwa mtu fulani ambaye wewe humjui. Kama hazina yako imejificha kwa mtu huyo usiyemjua, ndio kikwazo kikubwa kinachokuzuia kufikia pengine mafanikio kwa kiasi kikubwa sana.

Wapi ilipo hazina ya mafanikio yako?
Hata pia inawezekana hazina yako imejificha kwenye changamoto ya aina fulani iliyo kwenye maisha yako. Kitendo  cha wewe kushindwa kuvumbua changamoto hiyo na kuipa majibu sahihi basi ni kikwazo kimojawapo kinakuzuia kufanikiwa.
Naweza kusema pia inawezekana hazina yako imejificha kwenye mji au kijiji fulani ambacho wewe hukijui. Siku utakapokijua kijiji hicho au mji huo utashangaa mafanikio yako yakimiminika kama maji na ukashindwa kuyazuia.
Upo uwezekano pia hazina yako kubwa ya mafanikio imejificha kwenye biashara ya aina fulani, ambayo biashara hiyo bado hujaanza kuifanya mpaka sasa, lakini ukiangalia kweli kwenye biashara hiyo ndio hazina yako ilipo.
Yapo maeneo mengi ambayo hazina yako inaweza ikawa imejificha, lakini wewe haujui. Unachatakiwa kufanya ili kuweza kugundua hazina yako pale ilipo ni wewe kuwa mtulivu, kufanya kazi kwa bidii, kuongeza ubunifu na kuishi na watu vizuri wanaokuzunguka.
Ukumbuke hazina yako ya mafanikio ilipo, haipo nje ya dunia hii, hazina yako ipo hapa hapa duniani unachotakiwa kufanya ni kuigundua ilipo. Kila siku katika maisha yako tamani kujua ni wapi hazina yako ilipo ya mafanikio. Usikubali kutoka katika dunia hii ukiwa mtupu wakati una hazina ya kutosha ya kimafanikio.
Najua unaweza ukawa unajua kuna watu ambao ulikuwa unawafahamu na ambao maisha yao yalikuwa magumu sana, lakini mara baada ya kufanikiwa kupata hazina zao zilipo, watu hao walipiga hatua kubwa sana ya kimaisha mpaka inashangaza.
Kama upo kwenye mateso ya kimaisha unaona kila kitu hakiwezekani kwako, nikwambie tu inawezekana bado unateseka kwa sababu hujui hazina yako ni wapi ilipo. Kitu cha kufanya endelea kuchapa kazi, wakati utafika utajua hazina yako ilipo.
Hata uwe maskini vipi au hujiwezi vipi kimaisha , siku ukijua hazina yako ilipo nakwambia duniani yako itabadilika na kuwa nyingine tofauti na ambavyo unajijua wewe au watu wanavyokujua wewe kwa sasa.
Kikubwa kwa imani yako mwombe Mungu akusaidie kujua ni wapi hazina yako ilipo ya mafanikio na huku ukiendelea kufanya kazi kwa bidii. Lakini kitu cha kufahamu sasa hazina yako ipo, unatakiwa kuitafuta na kuifanyia kazi ili uweze kufanikiwa.
Inawezekana unateseka sana kwenye maisha yako, kwa sababu bado hujui hazina yako pale ilipo. Siku ukiijua hazina yako ilipo, huo ndio utakuwa mwanzo mkubwa sana wa mabadiliko ya maisha yako kwa ujumla.
Naamini ukifanyia kazi na kuongeza juhudi kila siku, muda utafika utagundua ni wapi pale hazina yako ilipo. Fanyia kazi ujumbe huu wa leo kwako na umshirikishe mwingine aweze kutambua ipo mahali hazina ya mafanikio yake.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.