google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 10, 2018

Kama Usipozijua Hali Hizi Vizuri, Utakuwa Mtu Wa Kuumizwa Sana Kwenye Maisha.

No comments :
Katika maisha, zipo siku ambazo unakuwa umejawa na tabasamu na furaha tele, kutokana na mambo yako wewe kuweza kwenda vile kama unavyotaka. Halikadhalika, zipo siku ambazo zinakuwa za kilio na majonzi pengine kutokana na mambo kwenda hovyo.
Hali hii ya kufurahi na kuona kila kitu sawasawa kwa sababu ya mambo yanatuendea vizuri ipo na hali ya kuhuzunika wakati mambo yanakwenda vibaya pia ipo na tunakutana nayo kwenye maisha. Kila mmoja wetu amewahi kukutana na hali hizi.
Kama iko hivyo, unachotakiwa kujifunza ni hiki, wakati mambo yako yanakwendea vizuri, furahi kwa wakati huo. Pia wakati mambo yako yanapokwendea vibaya jenga uvumilivu, jikaze na amini wakati mzuri tena kwako unakuja.
Kosa kubwa wanalolifanya watu wengi, ni pale hali za kushuka zinapotokea kwao, ukizingatia hali hizi huambatana sana na maumivu makubwa, ni kule kujisahau na kuona kwamba kama wameonewa au hawakustahili kabisa kupatwa na hali hizo.



Maisha yamejaa hali za kupanda na kushuka sana. Kama ikiwa bado hujabaini kwamba kuna kushuka na kupanda kwenye maisha kila wakati, basi kila unapokutana na matukio hasi, utakuwa ni mtu wa kuumizwa sana.
Ukiangalia chanzo cha watu wengi kuumia na kuteswa na maisha ni kwa sababu ya watu hawa wao kujua maisha ni kupanda tu na hakuna kushuka. Watu hawa likitokea tukio dogo tu la kushuka huwaumiza sana na kuwatoa nje ya mwelekeo wao.
Watu wa namna hii kama ana biashara akipata hasara kidogo inamuuma sana na anaweza kuifunga. Akikwaruzana na mpenzi wake pia inauma sana nakuona karibu kila kitu hakifai. Anasahau kabisa kwamba maisha ni kupanda na kushuka.
Elewa ikiwa unataka kuishi katika dunia hii kwa amani na furaha, unatakiwa kujua maisha ni kupanda na kushuka. Kwa hiyo inapotokea kupanda, wewe furahi, lakini unapoona wakati wa kushuka jikaze na vumulia maumivu yote yanayoendana na kushuka huko.
Kikubwa unachotakiwa kukumbuka kwenye kushuka huko ambako kunaambatana na maumivu mengi hakutaweza kukupata wewe moja kwa moja. Hata itokee umeumia na kulia vipi, wakati wako wa kupanda utakuja pia.
Ikiwa kungekuwa hakuna kushuka, basi kupada juu kusingekuwepo. Ikiwa kungekuwa hakuna kupoteza, basi kufanikiwa na kushinda kusingekuwepo. Yote hayo yapo kiasili ili kukupa nguvu na hamasa ya kuweza kuendelea mbele.
Hata kama imefika wakati unaona giza totoro na hakuna tumaini lolote la maisha yako, tambua kabisa asubuhi yenye nuru inakuja na hakuna ambaye atakuwa mtu wa kukuzuia, hivyo usikatishwe na tamaa kwa hilo.
Haijalishi ni kitu gani ambacho umekutana nacho kwenye maisha yako. Haijalishi siku yako imekwenda vipi. Kikubwa unachotakiwa kujua zote hizo ni hali ambazo unatakiwa kuzitambua ili uishi maisha ya ushindi na furaha.
Kila wakati weka akilini kwamba maisha yana kupanda na kushuka. Hizo ni hali ambazo zipo. Usiruhuu hata kidogo hali yoyote ikuumize kupitiliza. Jifunze kukabiliana na kila hali kwa wakati wake ili usiweze kupoteza mwelekeo kwenye maisha yako.
Amua leo kuwa mtawala bora wa hali hizi zote mbili. Ukiweza kuzitawala vizuri hali hizi, basi maisha yako yatakuwa na furaha na amani nyingi na hautaweza kushi kwa majuto ya kupitiliza kama wengine wanavyoishi hivyo.
Kila kitu kinawezekana, tafakari na chukua hatua.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.