Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, August 8, 2017

Njia Ya Uhakika Ya Kukufikisha Kwenye Mafanikio Ipo, Kama Utafanya Mambo Yako Hivi...

No comments :

Kufanya kitu chochote hadi kikaonekana kuwa bora, hakutokei tu kwa bahati mbaya, bali kitu chochote bora kinakuja kwa gharama zake. Ili kufikia ubora wa kitu chochote ukifanyacho, elewa unahitaji ujasiri na kujitoa sana.
Kuna wakati unapotafuta yale yaliyobora maishani mwako utajikuta unakutana na upinzani na kujiona kama unarudi nyuma, lakini yote hayo yasikutishe hizo ni moja ya gharama ambazo unatakiwa ulipe.
Hata hivyo ukumbuke, njia ya uhakika ya kukufikisha kwenye utajiri ipo kwa wewe kufanya mambo yako kwa ubora. Kama kuna vitu unalipua lipua, unafanya ilimradi tu ufanye, hata kama kwa sasa unaona vinakupa mafanikio, lakini hutafika mbali.
Kama unataka kufanikiwa katika nyakati hizi, wewe kazana kuwa bora, kazana kuwa mbobezi, kazana kuwa ‘master’, kwa kila unachokifanya. Hata kama dunia haitaki ufanikiwe, ukizama na kubobea itakupisha tu na mafanikio utayapata.

No comments :

Post a Comment