google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 16, 2017

Hii Ndiyo Nguvu Kubwa Ya Mafanikio Unayotembea Nayo Kila Siku.

No comments :
Ipo nguvu kubwa ya mafanikio ambayo ukiamka unayo, popote unapokwenda pia ipo na inakufuata, nguvu hiyo ipo iwe unaijua au huijui ila ipo.
Nguvu hii ya mafanikio, kwa kuwa ipo karibu na wewe haimaanishi ni lazima kukufanikisha wewe, la hasha, nguvu hii inakufanikisha ikiwa utaitumia.
Kwa wale wote wanaoielewa na kuitumia kweli inawafanikisha, lakini kwa wale ambao hawaielewi hakuna wachofanikisha zaidi ya kuendelea kushindwa.
Najua unajiuliza nguvu hii ninayoiongelea ni nguvu ipi,  ni nguvu kweli au leo unaniona kama nimekuwa mzushi kukwambia kitu ambacho hakipo?

Kuwa na uchaguzi sahihi kila siku wa maisha yako, utafanikiwa.
Sikiliza rafiki yangu, nguvu kubwa ya mafanikio ambayo ninaizungumzia na hata wewe ukiitumia itakufanikisha, nguvu hii ipo kwenye uchaguzi unaoufanya kila siku.
Naona unatoa macho, ngoja nikwambie, chochote unachokifanya duniani ni matokeo ya uchaguzi wa aina fulani hivi kwenye maisha yako.
Kila kitu unachokiona duniani ni matokeo ya uchaguzi, kwa mfano maisha uliyonayo, ni matokeo ya uchaguzi wako utake au usitake.
Hakuna mtu katika hali ya kawaida anayekulazimisha kufanya jambo au kitu fulani, unaona kila kitu unachagua wewe mwenyewe.
Wewe ni kila kitu katika maisha yako, hakuna anayeweza kukuiingilia kwa lolote, una uwezo wa kufanya chochote ukitakacho na wakati wowote.
Hakuna atakayekulazimisha uamke asubuhi na mapema, hakuna anayekulazimisha uwekeze, yote haya yanabaki mikononi mwako kwa sababu ya nguvu ya uchaguzi.
Pia hakuna anaye kulazimisha utoe sababu ya kufanya au kutokufanya jambo fulani, ni wewe ndiye unayechagua kipi cha kufanya.
Kama hupendi hapo ulipo, chagua kile unachokipenda na kukifanya kwa juhudi zote hadi utoke hapo na kukaa sehemu unayoipenda.
Kwa nini unaendelea kusubiri kuumizwa na ugumu wa maisha na hutaki kuchukua hatua? hebu chukua hatua za kukutoa hapo ulipo. Hatua ni kitu muhimu sana kwako.
Kama nilivyosema, nguvu ya uchaguzi ya kuchagua kitu chochote ipo mikononi mwako. Hakuna anayeweza kukuzuia kuchagua kitu, maisha yako umeyachagua mwenyewe.
Kila wakati unatakiwa uelewe uchaguzi unaoufanya ndio unaamua maisha yako yawe ya namna gani. Una uchaguzi mbovu basi maisha yako yatakuwa mabovu pia.
Kumbuka uchaguzi ulionao na unaofanya kila siku hata kwenye vitu vidogo vidogo, hiyo ndiyo nguvu kubwa ya mafanikio ambayo unayotembea nayo ya kimafanikio.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.