Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, August 10, 2017

Ukomavu Katika Maisha Yako Unajengwa Hivi...

No comments :

Ukomavu katika maisha hauji katika kipindi ambacho mambo yako ni safi au una raha zote. Ukomavu katika maisha yako unakuja kile kipindi ambacho unakutana na changamoto nzito sana ambazo zinakuacha hata ulie au uhuzunike.

Wabeba vyuma wanajua, ili kujenga misuli imara haukuji hivi hivi tu, ni lazima kunyanyua vyuma kila siku tena kwa nguvu zote. Hali hii iko hivyo pia hata katika maisha yako, ukomavu wako unajengwa na changamoto unazopitia.

Changamoto zinakupa kitu fulani cha kufanya, zinakufanya ukue na utoke hapo ulipo na kwenda sehemu nyigine ya kimafanikio. Hali yoyote ngumu unayokutana nayo katika maisha yako jifunze kuiona nayo kama fursa ya kimafanikio.

No comments :

Post a Comment