google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 27, 2017

Sababu Mbili Zinazofanya Wengi Washindwe Katika Maisha.

No comments :
Najua unaelewa vizuri kwenye maisha kundi kubwa la watu wanaonekana wameshindwa maisha au wameshindwa kufanikiwa kwa viwango vya juu ukilinganisha na kundi dogo la watu ambalo ndilo limefanikiwa.
Kutokana na matokeo hayo ya kundi kubwa la watu kushindwa katika maisha, kundi hili kihalisia, hujikuta likianza kumwaga sumu sana kwa wengine wanaotaka kwenda juu. Sumu hizi zinaweza zikawa za maneno na kila namna ya kukatisha tamaa.
Kwa hiyo inapotokea unapingwa sana kwa kile unachokifanya, hutakiwi kushangaa wala kuhoji sana, ni kwa sababu unaishi na upo na jamii ambayo imeshindwa sana, sasa kitu cha kujiuliza unafikiri watu hao watakwambia nini zaidi ya kukukatisha tamaa?

Ukiwa na sababu katika mafanikio, utashindwa tu.
Ni ngumu sana kuweza kukwepa kupingwa, kubezwa, na hata kudharauliwa kwamba huwezi kitu ikiwa unaishi kwenye jamii kubwa inayokuzunguka ambayo mafanikio kwao ni msamiati au ni kitu ambacho hakiwezekani.
Kitu kingine ambacho ninatakiwa nikiulize wewe rafiki yangu, hivi umeshawahi kujiuliza nini hasa chanzo au sababu inayopelekea kuona watu wengi wakiendelea kubaki katika hali duni kwa muda mrefu sana? umeshawahi kujiuliza kwa nini hiyo iko hivyo?
Kama hujawahi kujiuliza kwa nini hiyo iko hivyo, leo nataka nikushirikishe sababu au mambo mawili tu ambayo yanawafanya wengi washindwe sana kwenye maisha. Hata kama wewe unafanya mambo hayo na utaendelea kuyafanya, hutakwepa kushindwa.
Jambo la kwanza, ni kuishi kwa kutoa sababu sana/visingizio.
Wapo watu ambao naweza nikasema maisha yao yote wameamua kuwa ni watu wakutoa visingizio. Watu hawa ni wagumu sana kuchukua hatua ila wakiulizwa kwa nini hawajafanya, wanasababu nzuri sana za kujitetea kwa nini hawajafanya hicho kinachotakiwa kufanyika.
Siku hadi siku zinasonga, lakini utawakuta watu hawa wako pale pale, watakwambia hawajawekeza kwa sababu wanasomesha, pia watakwambia hawajawekeza bado wanajipanga na sababu nyingine kama hizo.
Kwa kawaida ili kufanikiwa kila sababu unatakiwa uiweke pembeni, unatakiwa ubaki wewe kama wewe. Kuendelea kuwa na sababu ni kitu ambacho kamwe hakitakuja kukusaidia katika maisha yako zaidi kitakuangusha. Weka sababu pembeni,utimize ndoto zako.
Jambo la pili, kukosa nidhamu.
Mbali na kuishi kwa kutoa visingizio sana, wapo watu ambao wanashindwa kwenye maisha kwa sababu ya kukosa nidhamu. Watu hawa ukichunguza maisha yao karibu yote, hawana nidhamu ya kila kitu.
Utakuta wa ndio wanaongoza kwa kukosa nidhamu ya pesa, wao ndio wanaoongoza kwa kukosa nidhamu ya muda na pia wanaongoza kukosa nidhamu ya kazi. Sasa watu wa namna hii inakuwa ni ngumu au muujiza kwao kufanikiwa.
Kwa kuhitimisha tunaona, mambo makubwa yanayowaangusha wengi kufikia mafanikio ni kukosa nidhamu na kutoa visigizo sana. Ni jukumu lako yashughulikie mambo hayo ili na wewe yasije yakakuangusha kwenye maisha yako.
Nikutakie mafanikio mema na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza maisha na mafanikio kila siku.
DAIMATUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.