google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 14, 2017

Mambo Manne Yatakayokusaidia Kuokoa Muda Wako Wakati Wote.

No comments :
Kati ya kitu ambacho ni changamoto kwa wengi sana ni swala la muda. Kwa watu wengi kutunza muda na kuutumia kwa manufaa imekuwa ni changamoto kubwa na kwa bahati mbaya wengi wanaopoteza muda sana wanaona ni kitu cha kawaida.
Madhara ya kupoteza muda yamekuwa hayaonekanai moja kwa moja, lakini nikwambie tu hivi kupoteza muda na kuamua kuutumia hovyo, hiyo ni zaidi ya kupoteza pesa au kwa lugha nyingine ndio unapoteza maisha yako.
Unaweza ukajiuliza kwa nini ninasema hivyo? Hiyo iko hivyo kwa sababu ukipoteza muda wako sasa hata kama ni dakika moja, hauwezi kurudi mpaka unaiacha hii dunia. Kwa msingi huo, unatakiwa kutunza sana muda wako kuliko kitu chochote.
Na swala la kutunza muda haliji kwa bahati mbaya, yapo mambo ya msingi sana ambayo kama umedhamiria kweli kuutunza muda wako unatakiwa uyafatilie kwa makini ili yakusaidie kutunza muda wako kwa usahihi.

Tunza muda wako vizuri ukupe mafanikio.
Jambo la kwanza, hamasa.
Hapa ni lazima kweli uwe na hamu au nia ya kutunza muda wako. Kitu cha kwanza ambacho kitakuwa kinachemka ndani yako kwako ni kwa wewe kutaka kuona lile kusudi kutunza muda linatimia  tena kwa uhakika.
Ukiwa una nia au shauku ya kweli ya kutunza muda wako, hii ni hatua ya kwanza kabisa ambayo utakuwa unaanza nayo na ambayo itakuwa kama msingi wa kukusaidia kuweza kutunza muda wako kwa uhakika.
Jambo la pili, tafuta mwelekeo sahihi.
Huwezi wewe ukawa mtunza muda mzuri, halafu ukawa hujui au huna mwelekeo sahihi. Unatakiwa ujue mwelekeo sahihi wa kazi zako kwa siku, kwamba zitakwendaje, utafanya nini wapi na wakati gani.
Ili kufanikiwa katika hili hutakiwi kuanza siku yako bila kujua siku inayofuata utafanya nini wapi na kwa wakati gani. Weka ratiba yote ya mambo yako ambayo unatakiwa kuyatekeleza kwa siku husika na uyafatile, hapo utaokoa muda wako.
Jambo la tatu, maamuzi sahihi.
Tunaona hapa kuwa na mwelekeo sahihi na hamasa ya kutunza muda peke yake hiyo haitoshi, unatakiwa kuongeza kitu cha ziada ambacho ni kuwa na maamuzi sahihi. Lazima maamuzi yako yawe sawa. Ukiwa na maamuzi ya kutanga tanga, utapoteza muda wako sana.
Ni muhimu hapa kujua unatakiwa kufanya kitu gani wapi na wakati gani.  Unapojijengea maamuzi sahihi, utajikuta unaokoa muda wako mwingi ambao pengine ungeweza kupotea bila sababu ya msingi kwako.
Jambo la nne, nidhamu binafsi.
Itakuwa ni kazi bure kufanya mambo yote tuliyotangulia kuyaongea kama huna nidhamu binafsi. Unatakiwa uwe na nidhamu binafsi katika kutekeleza majukumu yako kama ulivyoyaweka kulingana na siku hiyo.
Kwa kuzingatia mambo hayo, itakuwa ni silaha tosha kwako wewe ya kuweza kukusaidia kutunza muda wako vizuri na kwa uhakika mkubwa. Ikitokea kama hautafanya  hivyo sahau kutunza muda na utaendelea kuupoteza.
Chukua hatua, kila la kheri katika kufikia mafanikio yako na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila wakati.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.