Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, August 7, 2017

Kama Utayajua Mambo Haya Vyema, Sahau Kushindwa Hovyo Kwenye Maisha Yako.

No comments :
Maisha yako ni matokeo ya uchaguzi wako, hili ni jambo ambalo tumekuwa tukilitia sana mkazo hapo kwenye DIRA YA MAFANIKIO karibu kila wakati.
Kutokana na maamuzi unayofanya kila siku, maamuzi yanakufanya pia uchague kuishi maisha ya aina fulani, haijalishi maisha hayo ni mabaya au mazuri.
Kwa mfano tunaona, kutokana na maamuzi yako inakupekea kuishi maisha ya kipato fulani, au inakupelekea kuishi katika hali fulani na marafiki wa aina fulani.
Hebu angalia pale ulipo maisha uliyonayo na vitu vile vinavyokuzunguka au unavyovimiliki, unaona vinakupa picha au matokeo ya maamuzi yako.

Kama hapo ulipo una pesa nyingi uelewe kabisa uliamua kuwa na kiasi hicho cha pesa kutokana na maamuzi ambayo ulikuwa ukiyafanya karibu kila siku.
Kama hapo ulipo umechoka huna kitu na mifiko imechacha kabisa pia elewa kabisa ni matokeo ya uamuzi uliochukua, huhitaji kubisha katika hili huo ndio ukweli.
Maamuzi yako yana uwezo wa kusababisha ukachagua kuishi maisha ya aina fulani, hivyo kila wakati unatakiwa kuwa makini na mwangalifu sana na maamuzi yako.
Kila jambo unalotaka kulifanya, jiulize mara mbilimbili, jambo hilo linakupa manufaa au linakupotzea muda na baadae ikawa ndio chanzo chako cha kuweza kushindwa?
Fanya kila kitu kwa mahesabu mazuri, fanya mambo yako kwa kujua kabisa kwamba unatakiwa kufanya maamuzi sahihi na uchaguzi sahihi vyote kwa pamoja.
Maisha yako yanahitaji maamuzi ya busara, yanahitaji pia uchaguzi wa busara ili au kukupa mafanikio, kinyume cha hapo utashindwa.
Hiyo ikiwa na maana kwamba kila kitu unachotaka kufanya unatakiwa angalia sana sababu kubwa mbili, yaani maamuzi na uchaguzi.
Ukizingatia sababu hizo mbili kila unapofanya kitu sio rahisi kuweza kuanguka., lakini ukumbuke sababu yako ya kwanza iwe uamuzi, kisha uchaguzi.
Ukijichanganya na ukajivuruga hapo, utakuwa ni mtu wa kulia sana kwenye maisha yako kwani maamuzi yako na uchaguzi wako kila wakati vitakuwa ndio vinakuangusha.
Kuwa makini sana katika hili na hakikisha unachukua hatua thabiti zitakazoweza kukusaidia kuboresha maisha yako leo kuliko ilivyokuwa jana.
Nikutakie siku njema na kila kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAMAIRIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
No comments :

Post a Comment