google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 30, 2017

Hapa Ndipo Mafanikio Yako Makubwa Yanapoanzia.

No comments :
Ni rahisi kuwaza na kutafuta sana pale mafanikio yako makubwa yanapoanzia. Hata hivyo pamoja na kuwaza huko kote bado wengi wanazunguka, hawajui sana mafanikio yao makubwa yanaanzia wapi?
Leo kupitia makala haya, nataka nikuonyeshe chanzo cha mafanikio yako makubwa yanaanzia wapi. Ni ngumu sana kuweza kufanikiwa na kufika ngazi kubwa ya kimafanikio kama huelewi vizuri mafanikio yako makubwa yanaanzia wapi.
Kwa kawaida, mafanikio yako makubwa yanaanzia kwenye ile imani uliyonayo juu ya mafanikio hayo makubwa unayoyataka. Hutaweza kufanikiwa sana zaidi ya ile imani uliyonayo. Imani yako ndio kila kitu na dawa ya mafanikio yako makubwa.

Jenga imani sahihi ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Unapokuwa unaamini kwamba unaweza kufikia mafanikio yako fulani, unajikuta kutokana na imani hiyo unaanza kuchukua hatua za kukufikisha kwenye kile unachokiona kwenye akili yako. Imani yako inakuwa inakusukuma kufanya zaidi na zaidi hadi kufanikiwa.
Hapa imani yako naweza nikasema inasimaama kama taa ya kuweza kukuongoza wapi uweze kufika kimafanikio. Hiyo ikiwa na maana kama ukiwa na imani hafifu, imani ambayo siyo kubwa huwezi pia kufanikiwa sana.
Kumbuka ninachotaka hapa unielewe, nazungumzia imani yako kama dawa pekee ya kukufikisha kwenye mafanikio yako. Na unielewe pia hapa sizungumziii tumaini, nazungumzia imani yako.
Ipo tofauti kubwa sana kwa mtu anayeishi kwa matumaini na mtu anayeishi kwa imani. Yule mtu anayeishi kwa matumaini anaweza asichukue hatua yoyote lakini akajipa matumaini atafanikiwa kitu ambacho sio kweli.
Ili kufikia mafanikio uyatakayo, unatakiwa kuwa na imani sahihi ya mafanikio yako. Imani hii tunaweza tukasema ni imani ya kumudu, imani ya kuamini kwamba unaweza kufanya kitu fulani na kweli ukachukua hatua hata kuweza kufanikiwa kwenye kitu hicho kwa uhakika.
Unapokuwa na imani, unakua unaona mambo kwa utofauti, unakuwa unachukua hatua zako kwa utofauti na inakuwa sio rahisi kwa mtu mwenye imani inayooendana na kuchukua hatua kuweza kukata tamaa mapema. Wanaokata tamaa mapema ni wale wanaoishi kwa matumaini sana.
Kipi unachotakiwa kukifanya leo ili kujenga mafanikio yako, ni kwa wewe kujenga imani ya mafanikio. Amini kwamba unaweza kuchukua hatua sahihi, usijaribu kuishi kwenye matumani utakuwa unajitengenezea mazingira ya kushindwa.
Hakuna mafanikio makubwa yanayoanzia nje ya imani uliyonayo. Utafika tu pale kwenye mafanikio yako kutokana na imani inayokuongoza ndani mwako na sio vinginevyo.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Kila la kheri katika kufikia mafanikio  makubwa,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.