google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 22, 2017

Hivi Ndivyo Utandawazi Na Teknolojia Vinavyofanya Kazi Katika Sayari Hii Ya Wasakatonge.

No comments :
Ukuajaji wa utandawazi pamoja na teknolojia kwa namna moja au nyingine umetusaidia kuweza kupima kiwango cha maendeleo ya dunia na jamii kwa ujumla. Kiwango hicho cha maendeleo kitokanacho na utandawazi kimekuwa kikipimwa siku hadi siku.
Utandawazi huo huo pamoja na teknolojia umesadia kuweza kuipambanua dunia ya zamani na dunia ya sasa. Kutoka na mabadiliko hayo ndipo tunapopata hadithi zama za kale za mawe, na sasa tupo zama za tekolojia na ukuaji wa utandawazi.
Kiuhalisia ni kwamba zama hizi za tekinolojia na ukuaji wa utandawazi zina faida lukuki sana hasa kwa wale wenye kujua namna ambavyo wanaweza kuendana na zama hizi, lakini wengi wate ambao hatuwezi kuendana na zama hizo, tumekuwa wakipata hasara tu.
Tunaweza tukajikita hata kwa dakika chache kuwaza, hivi kwa mfano ugunduzi wa simu, kompyuta za kisasa pamoja na ujio wa mitandao ya kijamii inakusaidia wewe na kwa kiwango gani? Au unaiona ipo ipo tu.

Hivi Ndivyo Utandawazi Na Teknolojia Vinavyofanya Kazi Katika Sayari Hii Ya Wasakatonge.
Tumia teknolojia vizuri ikufanikishe.
Bila shaka wengi hatujui ni kwanamna gani vitu hivyo vitavyoweza kutusadia sisi kuweza kufika mbali kimafanikio, wengi tunachukulia ujio wa teknolojia ni kama kuifurahisha tu akili zetu.
Wakati mwingine tunadhani ya kwamba ugunduzi wa mambo mbalimbali katika sayari hii ni kwa ajili ya watu wachache tu, la hasha kila kitu ni kwa ajili ya watu wote madharani wewe unayesoma makala haya. Hivyo kila kitu kilichopo zama hizi lazima ukiwazie kinakupaje wewe fedha.
Kila kitu ambacho unakiona katika ulimwengu huu wa utandawazi kina faida na hasara zake, ila wengi wetu tumekuwa tunavitumia vitu hivyo kwa upande wa hasara zaidi huku tukipumbazwa na kuona hasara hizo ndizo faida.
Kama upo katika katika upande wa kuona hivyo, tafadhari nakuomba ufanye mapinduzi kwani dunia ya sasa imebadilika sana, kile ambacho unakijua leo, upo uwezekano  kitakuwa hakina thamani siku ya kesho.
Ukuaji wa wa utandawazi ndio ambao umeleta maana hiyo. Hebu tujiulize kidogo na kuona maajabu ya teknolojia jinsi ambavyo yanafanya hicho ambacho unakijua leo kinavyokuwa hakina thamani siku ya kesho.
Hebu tujiulize wale waliokuwa wanafanya kazi kwa kutumia ‘typwriter’ na leo utandawazi umeleta kompyuta, wale watu waliofanya kazi kwa ‘typwriter’ wanafanyakazi gani? Bila shaka utagundua ya kwamba watu wa ‘typwritter’ watashindwa kuendana na kasi hii ya teknolojia.
Tuendelee kujihohoji wale ambao walikuwa wanafanya kazi za uhasibu hapo awali, ambapo kazi hii kila mtu akipeenda na leo hii karibu kila kampuni watu wanafanya miamala kwa kutumia simu, hawa wahasibu wanafanyakazi gani? Bila shaka utagundua ya kwamba kazi nyingi ambazo zilikuwa zinafanywa na watu mbalimbali kwa sasa zinapungua na kufanywa na mashine.
Zipo kazi nyingi sana ambazo leo zimerahisishwa sana, badala ya kufanywa na watu , zimekuwa zikifanywa na mashine, kwa mtindo huu naendelea kuwaza kwa sauti hivi hicho ambacho unakijua leo kesho kitakuwa na thamani tena? Bila shaka majibu unayo mwenyewe.
Hivyo kwa kuwa mabadiliko makubwa yanayoendelea kufanyika katika sayari hii yanafanya mambo makubwa kutokufanywa na wewe, unachotakiwa kufanya ni kujiongeza kwani zama zimebadilika sana.
Hivyo jijengee mifereji mingi ya kuweza kujua vitu vingi zaidi ya hicho ambacho unakijua sasa, kujua vitu vingi kutakufanya uweze kujua namna ya kuweza kuishi kesho.
Maisha yanabadilika sana hivyo ni heri kila wakati kuweza kuwa bora zaidi kwa kile ambacho unachokifanya acha kung'ang'ana na mambo ya mwaka 47, kwani hayana tena thamani tena mbele ya sayari hii, na hata kama yatakuwa na thamani kinachohitajika ni kuweza kujifunza namna ya kukiboresha kitu hicho ili kuendana na kasi ya sayari hii.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada, tukutane siku nyingine.
Ndimi afisa mipango, Benson Chonya,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.