google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 18, 2017

KITABU; The Time Management (Matumizi Mazuri Ya Muda).

No comments :
Katika kitabu hiki cha THE TIME MANAGEMENT, mwandishi Brian Tracy anaonyesha umuhimu wa kuwa na matumizi mazuri ya muda ili kujihakikishia furaha na mafanikio ya kudumu kwa yale tunayoyafanya.
Mwandishi anaweka wazi bila ya kujijengea tabia ya kuwa na matumizi mazuri ya muda, basi maisha yako yatakuwa yanapotea sana pasipo kujua kwa nini iko hivyo. Hivyo anasihi kutumia muda vizuri kwa manufaa yetu ya leo na kesho.
Yapo mengi ya kujifunza kutoka kwenye kitabu hiki, lakini hebu tuangazie haya machache kwa kifupi na tujifunze pamoja.
1. Pamoja na kwamba kwa siku, juma, mwezi na hata mwaka una mambo mengi  kufanya, lakini jifunze kuchagua mambo matatu ya muhimu ambayo utayafanya kwa siku, wiki, mwezi na hata mwaka mzima. Mambo hayo matatu ndiyo yawe muhimu na kuyawekea vipaumbele vya hali ya juu sana.
2. Washindi katika maisha siku zote wanatumia muda wao vizuri, wale wanaoshindwa katika maisha siku zote wanatumia muda wao hovyo. Ili kuthibitisha hili, angalia watu wenye mafanikio wanatumia muda wao vipi na washindwaji wanatumia muda wao vipi.


3. Kama unataka kuwa na matumizi mazuri ya muda ni muhimu kujua matumizi mazuri ya muda wako yanakwenda wapi na yana maana gani kwako.
Hapa ina maanisha unakuwa unachagua aina ya maisha ambayo unatakiwa uyaishi kulingana na matumizi ya muda wao.
Wengine matumizi mazuri ya muda wao ni kufanya kazi kwa juhudi sana kutwa nzima na wakati wa usiku ni kulala usingizi mzito.
Wengine matumizi mazuri ya muda wao yapo kwenye kukaa na familia zao pamoja na kufurahia maisha.
Wengine matumizi ya muda wao ni kuongea na watu makini ambao wana msaada mkubwa wa maisha.
Inabidi ujue namna ya kuchagua mambo ya kufanya hasa pale unapokuwa na muda ambao umeupata. Ukishindwa kufanya hivyo utapoteza sana muda wako.
4. Kila siku ieleweke kwamba yapo majukumu ambayo yanatakiwa kutekelezwa. Linapokuja swala la majukumu, kuna majukumu makubwa ya aina tatu;-
Majukumu muhimu na ya lazima, hapa kwa mfano kuongea na wateja, kutekeleza kazi uliyojiwekea kwa siku au kulipia ‘bill’ inayotakwa kukatwa.
Majukumu muhimu lakini sio ya lazima, katika majukumu haya inaweza ikawa ni kusoma masomo mapya kwa baadae au kununua nguo.
Kuna mjukumu ambayo siyo ya muhimu na sio ya lazima, majukumu haya inaweza ikawa kama kuangalia sinema, kutembea tembea hata kuongea soga zisizo za msingi.
Tatizo la watu wengi linakuja wanapoteza muda sana kwenye majukumu ambayo siyo ya muhimu kwao na pia sio ya lazima.
Ili kufanikiwa unahitajika sana kufanya majukumu ambayo ni ya muhimu kwako na pia ya lazima kwenye maisha yako.
5. Kati ya kitu kibaya katika safari ya mafanikio ni kuahirisha mambo.kuahirisha mambo hiyo ni sawa na kujiibia muda wako wewe mwenyewe au kuahirisha mambo naweza nikasema hiyo ni sawa kuamua na kupoteza maisha yako mwenyewe.
Tofauti inayojitokeza kati ya waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa ni kwamba, waliofanikiwa wanairisha mambo kwenye yale mambo ambayo sio ya msingi, lakini wasiofanikiwa wanaairisha mambo yale ya msingi sana kwao.
6. Ili kufanya kazi zako kwa ufanisi, jifunze kugawa muda wako angalau kwa dakika 90 za kufanya kazi kwa uhakika. Ukifanya chini ya hapo unajidanganya na unajipotezea muda wako wingi bure.
7. Ili kuokoa muda wako, kama umeamua kufanya kazi fulani, ifanye na kuweka akili zako zote hapo. Maongezi ya simu au chochote kile kisiingilie kazi ambayo umeamua kuifanya kwa manufaa. Kama ni simu ongea maneno machache sana na ya faida.
8. Ili kuokoa muda wako, tenga muda wa kusoma e-mail zako, hakuna ambaye atakufa kama akituma e-mail akashindwa kusubiri angalau kwa siku moja. Jiwekee utaratibu wa kusoma e-mail hata kama ni kila saa kumi jioni. Kama kuna dharura, mtu huyo apige.
9. Ili kuokoa muda wako, jiwekee pia utaratibu wa kupokea simu na kuingia kwenye mitandao ya kijamii. Unaweza ukawa unaingia kila baada ya masaa 4 au zaidi ili kuokoa muda, hususani mitandao kama whats app, na mitandao mingine ya simu.
10. Ili kuokoa muda wako, usipokee simu zako hovyo, ‘usi-chat’ kwa meseji hovyo, usiongee kwenye simu muda mrefu sana, ongea agenda muhimu za kuweza kukusaidia. Matumizi ya hovyo ya simu ni upotevu wa muda.
11. Wekeza angalau saa moja kila siku kwa kusoma, ikiwa utawekeza angalau saa moja kwa kusoma, basi baada ya miaka mitano utakuwa upo juu sana kimafanikio na utakuwa ni miongoni mwa watu wenye mafanikio makubwa sana kwa wakati wako.
12. Moja ya matumizi mazuri ya muda ni kulala mapema na kuamka mapema kwa kufanya mambo yako kwa ufasaha. Unapolala mapema unapata muda wa kupumzisha mwili wako sana, na hali ambayo inakupelekea uamke ukiwa na hamasa mpya.
Chukua hatua kufanyia kazi haya muhimu uliyojifunza hapa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE, 
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.