google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 11, 2017

Jinsi Ya Kutengeneza Tambi Za Dengu.

No comments :
Karibu sana mpenzi msomaji wa blog hii ya dira ya mafanikio, lengo letu ni kuhakikisha kila mmoja anatimiza kusidio lake hapa duniani. Kama utakuwa ni mdau wetu mzuri tayari tumekwisha fundisha namna ya kutengeneza tomato souce, chill souce, karanga za mayai, tambi za mayai. Hivyo kwa kuwa tunajali uwepo wako kila wakati   siku ya leo tutajifunza namna ya kutengeneza  tambi za dengu.
Mahitaji:
1.    Unga wa dengu ½ kilo
2.    Binzari nyembamba ½ kijiko cha mezani
3.    Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai
4.    Unga wa mchele ¼ kilo
5.    Chumvi kiasi
6.    Mafuta ya alizeti ½ lita
7.    Baking powder

Namna ya kutengeneza
Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi. Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga. Changaya vizuri na kisha weka maji kidogo kidogo huku ukukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi. Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa moja.
Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa. Kisha chukua mashine ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni.
Weka kiasi kiasi huku ukikaanga. Acha mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Ipua na weka pembeni. Weka kwenye sahani safi na kavu. Tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Tafuta fingushio vizuri funga kisha peleka sokoni, wengine wataniuliza afisa mipango mashine hizi za dengu nazipata wapi? Wala usijali mashine hizi zipo nenda kwenye maduka ambayo yanauza vyombo mbalimbali vya mapishi kisha ulizia ya kwamba unataka mashine za kutengeneze tambi watakupa.
Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada tukutane siku nyingine, kama unahitaji masomo mengine kama haya ya ujasiriamali usisite kuwasilaina nasi.
Ndimi Afisa Mipango Benson chonya,
0757909942,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.