google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 9, 2017

Mbinu Mpya Za Kumfanya Mteja Kuwa Mfalme.

No comments :
Moja kati ya changamoto kubwa ya ufanyaji wa biashara ni kule kufanya kazi kwa mazoea, nasema hivi kwa sababu wafanyabiashara wengi husikika wakisema ya kwamba mteja ni mfalme, lakini katika hili kumekuwa na ukakasi ni wateja wachache sana ambao huuona ufalme huo.
Hii ni kwa sababu wafanyabiashara wachache sana ambao wamekuwa wakijua ni nini maaana ya mteja. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakimchukulia mteja pale anapokuja kwenye biashara ambayo anafanya tu. Kufanya hivi hufanya kuoina ramani ya biashara haina busara kwani biashara utazidi kuiona ni ngumu siku zote.
Hivyo ili uweze kumfanya mteja wako awe ni mfalme unatakiwa kufanya mambo yafuatayo;
1. Acha mara moja kumsubiri mteja wako aje kukufuata mfanyabiashara mahali ulipo, bali anza utaratibu wa kumfuta mteja wako mahali alipo, kufanya hivyo kutamfanya mteja wako ajisikie huru na pia ajihisi kuwa yeye ni mfalme kweli, na pia kufanya hivi kutamjengea utaratibu mpya na pia kujiona yeye si mteja tu kwako bali ni sehemu ya biashara yako.

2. Tengeneza utaratibu mpya wa kuwa na mawasiliano ya karibu na mteja wako, si umekuwa ukisema ya kwamba mteja ni mfalme, kama ndivyo hivyo basi hakikisha ya kwamba unakuwa na mawasiliano na wateja, mawasiliano haya chochonde naomba yawe ni kwa ajili ya biashara tu, kwani pindi ukiyatumia mawasiliano hayo kivingine basi jiandae kuwafukuza wateja wote ulionao. Mawasiliano haya yawe ni yale ya kuwajuza wateja kuhusu ujio wa bidhaa mpya.
3. Jifunze mbinu mpya ya kuweza kufanya mazungumzo na wateja. Hivi hujawahi kenda katika biashara ya mtu mwingine mpaka ukajuta ni kwanini ulienda mahali hapo, bila shaka kama hali hii imewahi kukutokea basi ni vyema katika biashara yako uweze kujenga utaratibu mpya ambao utakufanya wateja wako wajisiie huru kila wakija wako.
4. Uchawi mkubwa ambao unafanyika katika biashara ni kutoa ofa kwa wateja wako. Hii ni siri ambayo nakuibia wewe siku ya leo, haijalishi ni biashara gani ambayo unaifanya ila ili uweze kukua katika biashara hiyo ni vyema ukajiwekea utaratibu wa kutoa ofa katika biashara yako, jitahidi kutoa ofa kama yafanyavyo makampuni ya simu kufanya hivi kutawafanya wateja wengi waje kwako.
Asante sana kwa kusoma makala haya, mpaka kufikia hapo sina na ziada nikutakie siku njema na kazi njema.
Niliandika makala haya ni yuleyule wa siku zote, afisa mipango Benson Chonya.

0757909942,
bensonchony23@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.