google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 24, 2017

Misingi Mingine Ya Kuzingatia Wakati Unataka Kumjengea Mtoto Wako Nidhamu Ya Kweli.

No comments :
Kumlea mtoto katika nidhamu na maadili ni mojawapo ya jukumu kubwa sana kwa mzazi. Kila mzazi anapenda kumwona mtoto wake akikua katika maadili mema yatakayomsaidia katika maisha yake yote ya kesho.
Kutokana na kiu hii ya kila mzazi kutaka kuona mtoto wake akikua katika maadili bora, hapo sasa ndio kila mzazi huamua kutafuta njia au misingi bora ya kufuata katika kumlea mtoto hadi kuleta mafanikio.
Najua zipo njia nyingi au misingi bora ya kumlea mtoto hadi kuwa katika maadili bora. Lakini leo nataka tuangalie misingi mingine ambayo unaweza kuifuta na kumlea mtoto na kumjengea maadili bora kabisa.
Tunajifunza misingi hii bora kwa sababu, usipojua njia bora mapema ya kumlea mwanao unaweza kujikuta umekuwa kama polisi kwa mtoto wako na kupelekea mtoto hata kukukimbia bila sababu na kuona nyumbani pa chungu.
Bila ya kupoteza muda, hebu tuangazie dondoo kadhaa za kutusaidia mimi na wewe kuweza kujenga msingi imara katika malezi ya watoto wetu.

Misingi Mingine Ya Kuzingatia Wakati Unataka Kumjengea Mtoto Wako Nidhamu Ya Kweli.
Mlee mtoto wako katika njia njema impasayo.
1. Usimwekee mtoto sheria nyingi sana.
Itakuwa ni kosa kwa mzazi kumwekea mtoto wako sheria nyingi sana kwa kufikiri kwamba ndio unamjengea malezi bora. Kwa jinsi unavyomwekea sheria nyingi unamjengea mtoto hofu na kujiona yupo kama jela kumbe yupo nyumbani.
Kama ni sheria weka ila zisiwe nyingi. Hata hivyo unapoweka sheria hizo ambazo unazitaka, mweleweshe mtoto vizuri aelewe ni nini anachotakiwa kufanya ili ajue kabisa akivunja kuna adhabu fulani itafuata baada ya hapo.
2. Toa zawadi na acha kuadhibu sana.
Najua ukiwa kama mzazi kuna tabia ambazo unataka mtoto wako awe nazo. Tabia zile ambazo unataka mtoto wako awe nazo jifunze kumpa hamasa kwa kumwahidi zawadi fulani ili aziendeleze na ziwe tabia za kudumu.
Kwa mfano, kama hutaki mtoto wako atembee tembee hovyo na umeamua iwe hivyo, ikitokea akienda badala ya kumpa adhabu, anza kumwambia kwamba usipoenda labda kutembea na kukaa hapa na kusoma nitakununulia hiki au kile, hiyo itamsaidia pia.
3. Kuwa mzazi kiongozi.
Mwongoze mtoto wako katika kumwelekeza kujisomea, mwongoze katika mambo mbalimbali kama michezo na mengineyo, kwa jinsi utakavyokuwa ukimwongoza katika mambo hayo, mtoto wako ataelewa vizuri unataka nini na kufuata.
Ukiwa mzazi kiongozi, hata ule msingi imara unaoutaka wa tabia, utajikuta zinajengeka taratibu na hatimaye kuwa tabia zake za kudumu. Hakuna kinachoshindikana katika malezi ila kikubwa tumia njia sahihi na sio za kumuumiza mtoto.
Nikutakie ushindi katika malezi bora ya mtoto wako na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku juu ya maisha na mafanikio.
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.