google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 25, 2017

Maumivu Haya…Yasiwe Sababu Ya Wewe Kushindwa Kabisa Kwenye Maisha Yako.

No comments :
Kwenye maisha kuna wakati unaweza ukawa na maumivu ya kushindwa, kuna wakati unaweza ukawa una maumivu ya kupata hasara, kuna wakati unaweza ukawa una maumivu ya kuachwa na mwenzi wako au hata maumivu ya kuumizwa na chochote.
Maumivu kama haya yapo sana katika  maisha yako na yanapotokea maumivu ya namna hii ni rahisi kukuchanganya na kujiona kama vile umepoteza kila kitu kwenye maisha yako na pia hata ukaona maisha hayana maana.
Kosa kubwa ambalo hutakiwi kulifanya unapopatwa na maumivu haya ni kwa wewe kusimamisha shughuli zingine zikasimama huku ukiwa umekaa ukisikilizia maumivu hayo ambayo umekuwa umeumizwa.

Maumivu yako yasizuie ndoto zako.
Kitu unachotikiwa kuelewa maisha hayasimami, maisha yanaendelea kusonga mbele bila kujali umeumizwa au hujaamizwa. Inapotokea umeumizwa na kitu, acha kusimama au kuomba ‘poo’ endelea kupambana kwa nguvu zote.
Ikiwa itatokea ukakaa chini na kusubiria maumivu yapoe utakuwa ni mtu unayejichelewesha mwenyewe. Najua ni kweli maumivu ya kuachwa au kupata hasara fulani kubwa yanauma tena sana, lakini yasikufanye ukasimamisha shughuli zako.
Endelea na shughuli zako hata kama huku unalia kwa kuugulia hayo maumivu lakini usonge mbele. Ni bora ukawa unasonga mbele kidogo kidogo kuliko kusimama kabisa na kusikilizia maumivu yako.
Ni kitu kibaya sana kuamua kutulia kwa sababu ya maumivu yako. Inapotokea umeumizwa na jambo fulani chukulia jambo hilo kama somo lakini kubali kung’ang’ania kuendelea kumbana na hadi ufikie mafanikio yako.
Hapo ulipo kaa chini angalia ni kipi kinachokuumiza, ni kipi ambacho kimekufanya ukose tumaini kabisa, usichukulie kuumizwa huko wewe ndio basi huna kitu na huwezi tena kufanikiwa, hapana haiko hivyo.
Unayo fursa ya kufanya tena hicho kilichokuumiza na ukakifanya kwa mafanikio makubwa kuliko ya hapo ulipo. Nafasi ya pili ya kurekebisha makosa yako unayo na ukaendelea mbele zaidi.
Lakini hiyo haitoshi hata nafasi ya tatu, nne na tano ya kujirekebisha unayo. Kwa nini ujute na kuamua kukaa chini kabisa. Hebu shika mkono wangu na nyanyuka hapo ulipo na ukafanye kile unachotakiwa kukifanya cha kukupa mafanikio.
Kama nilivyosema maumivu yasiwe sababu ya wewe kushindwa kabisa. Chukulia maumivu hayo kama changamoto. Na kisha amua kwa dhati kutekeleza ndoto zako bila kujali ni nini au kitu gani kinatokea ndani mwako.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza maisha na mafanikio kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.