google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 4, 2017

Tabia Mbaya Za Fedha Zinazowaacha Wengi Kwenye Umaskini.

No comments :
Idadi kubwa ya watu linapokuja suala la pesa, wapo makini sana na  tabia kama kupanga mipango mizuri, kutumia pesa kwa busara na hata ikiwezekana kubana matumizi ili kuhakikisha usalama wa pesa unakuwepo.
Lakini, hata hivyo pamoja na wengi kijitahidi kufanya hivyo, bado zipo tabia ambazo watu wanazo zinawaacha au zinasababisha wengi kuendelea kubaki kwenye umaskini ingawa ukiangalia pia watu hao wana uwezo wa kupata pesa kila wakati.
Kwa hiyo hapa unaona tatizo la watu wengi sio kupata pesa, kama ni pesa kweli wanazipata, ila shida inakuja kwa kukumbatia tabia hizo ambazo zinawarudisha nyuma sana na matokeo yake kuwaacha katika dimbwi la umaskini.
Leo hapa katika makala haya, tunakuletea tabia mbaya ambazo kwa mtu yeyote akiwa nazo ni lazima mtu huyo ataendelea kubaki kwenye umaskini. Hakuna ujanja katika hili, kama una tabia hizi, nimesema utaendelea kubaki kuwa maskini.

Weka kumbukumbu ya pesa zako.
1. Kushindwa kuweka kumbukumbu ya matumizi yako.
Haijalishi unakipato kikubwa au una kipato kidogo, kuandika matumizi yako ni jambo la lazima ili uweze kufanikiwa. Kitendo cha kuwa na kumbukumbu na matumizi yako si suala la kumwachia Bill Gates peke yake hata wewe linakuhusu.
Huhitaji kutumia pesa zako tu hovyo kwa sababu eti unazo, unachotakiwa kujua ni wapi kila pesa yako inakwenda. Zoezi hili litakusadia sana kuwa makini na pesa zako na kukuokolea pesa nyingi ambazo zingepotea bila sababu.
Hili jambo liko wazi, hutaki kuweka kumbukumbu zako vizuri, utake usitake huwezi kutoka kwenye umaskini hata ufanyeje. Kama unabisha wafatilie watu wenye pesa nyingi sana, utaona hili wanalifanya sana maishani mwao.
2. Mhemko wa matumizi.
Tunaposema mhemko wa matumizi ni kufanya matumizi ya pesa kwa kutawaliwa na hisia zako. Hapa unakuwa unafanya matumizi kwa kuongozwa sana na hisia na unakuja kushituka kile kipindi ambacho pesa zako zimekwisha.
Kwa mfano, kwa sababu una pesa kila kitu kinachopita machoni mwako unataka unanunue, zizikipita nguo unataka kununua, kikipita kitu hiki au kile unataka kununua pia, huu ndio mhemko wa matumizi tunaouzungumzia hapa na ni tabia mbaya ya kipesa..
Watu matajiri wapo makini sana na matumizi yao, na hiki kitu hata wewe unatakiwa kuwa nacho ili kutengeneza utajiri wako. Pia kama hutaki kuwa makini na matumizi yako na kutawaliwa na mhemko, elewa utaendelea kubaki maskini.
 3. Kung’ang’ania njia moja ya kipato.
Kati ya hatari kubwa sana ambazo watu wengi wanacheza nazo na inawaacha kwenye umaskini ni kung’ang’ania kuendelea kuwa na njia moja ya kuengeneza kipato. Utakuta mtu anapata pesa nyingi kweli lakini njia ya kipato kimoja inamuangusha.
Najua unawajua watu ambao walikuwa wakifanya kazi kubwa na zenye mishahara mikubwa, lakini mara baada ya kuacha kazi unashangaa maisha yao yako hovyo sana. Yote hiyo inasababishwa na kuwa na chanzo kimoja cha kipato.
Labda tuseme hivi, utake usitake kama una njia moja ya kipato kuendelea kubaki maskini kunakuhusu kwa asilimia mia moja. Pigana na hali yako kwa kila namna uweze kutengeneza njia nyingne ya kutengeneza kipato, ndio utatoka..
4. Kukosa uvumilivu.
Sikuzote ili kupata pesa hakuji mara moja tu, ni zoezi ambalo linahitaji sana uvumilivu na kuchapa kazi kwa juhudi zote. Wengi wanashindwa kujua hili na kushindwa kuwekeza kwenye vitega uchumi ambavyo vingewapa pesa nyingi kwa baadae.
Kama unatabia za kutaka kupata pesa nyingi kwa chapu chapu na kushindwa kuwa mvimilivu sahau jambo hili. Unatajiri una kawaida ya kujengwa hatua kwa hatua hadi kufikia kilele kikubwa cha mafanikio.
Hizo ndizo tabia nne ambazo zinawaacha wengi kwenye umaskini, ingawa ule uwezo wa kupata pesa wanakuwa nao. Fanyia kazi hayo uliyojifunza, chukua hatua kila siku kuelekea kwenye mafanikio yako na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.