google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 23, 2017

Matajiri Wote Duniani Wanaanza Na Kitu Hiki, Hadi Kufanikiwa Sana.

No comments :
Kipo kitu kimoja ambacho kila aliyefanikiwa anaanza nacho hadi kufikia ngazi kubwa ya kimafanikio. Kitu hicho hata wewe unaweza ukawa nacho na ukikizingatia ni lazima utafikia mafanikio makubwa na kutakuwa hakuna cha kukuzuia.
Kitu hichi ndicho ambacho matajiri karibu wote duniani huwa wanaanza nacho na ndicho kinapelekea wao kuweza kufanikiwa na kufika pale walipo leo. Hakuna mwenye mafanikio makubwa sana ambaye hajaanza na kitu hicho.
Naona umetega sikio lako kisawasawa kutaka kujua kitu hicho ni kitu gani ambacho nataka kukiongelea hapa. Nakuomba usitie shaka, kitu ambacho nataka kukiongelea hapa ni kuanzia pale ulipo na kile kidogo ulicho.
Usishangae sana, kama nilivyosema karibu matajiri wote waliopo duniani safari yao ilianza na kidogo walichonacho au hawana kitu kabisa tena wengine wakitokea kwenye umaskini na wingi wa madeni uliwaofunika.

Anzia pale ulipo hadi kufikia kilele cha mafanikio.
Ukiangalilia matajiri kama Bill Gates, Warren Baffet, Larry Ellison, Michael Dell na Paul Allen wote hawa walianzia chini wakiwa na pesa kidogo, wakati mwingine hata ilikuwa ikiwalazimu kuishi katika madeni.
Matajiri hawa na wengineo, walipohojiwa nini siri ya mafanikio yao, wakati watu walioanza nao pamoja wamewaacha pale pale, ni wazi walidai sio kwa sababu ya akili au vipaji bali ni kujenga nidhamu binafsi na kuamua kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuliko mtu yoyote na tena kwa muda mrefu.
Kwa hiyo unaona kwao kuanza chini sio kitu ambacho kinawaogopesha. Kuanza chini wanachukulia kama changamoto tu ya kawaida ambayo mtu yeyote mwenye nidhamu na kujituma anaweza akaanzia huko na kufanikiwa sana.
Kwa mantiki hiyo, hata wewe unao uwezo wa kuanzia hapo ulipo na kufikia mafanikio makubwa sana. Kitu gani unachokiogopa hadi ushindwe kuanzia chini? Unaogopa kuchekwa au nini unachoogopa?
Tunaona karibu historia ya watu wote duniani wenye mafanikio walianza chini. Sasa wewe ambaye hutaki kuanzia chini eti unataka kuanzia juu nani kakwambia hivyo. Kila kitu kiasili kinaanzia chini na hatimaye kufikia mafanikio makubwa sana tena ya kutisha.
Ukiangalia kuanzia mimea, viumbe hai ni vitu ambavyo vinaanzia chini na mwisho wa siku kufikia mafanikio makubwa. Kwa hiyo, usijione kuna kitu ambacho utakosa sana kama ukianzia chini, anza na ulichonacho weka nidhamu na juhudi utafanikiwa sana.                     
Kuanzia leo usiwe na shaka na kitu chochote. Anzia maisha yako pale ulipo. Ndio, naamanisha hapo ulipo. Kila mtu anayeanzia chini anapata muda wa kujifunza na kukua, hatimaye kujenga mizizi mikubwa ya mafanikio yake.
Usijisikie vibaya au kujiona hufai kwa sababu unaanzia chini, anza na ulichonacho kutafuta mafanikio yako, anza na nguvu zako, anza na vipaji ulivyonavyo upo wakati utafika juu sana kimafanikio hadi utakuwa unajishangaa mwenyewe.
Ila kama unatafuta maisha ya juu, halafu hutaki kuanzia chini, mafanikio yako yatakuwa magumu sana kuweza kufikiwa.  Ni asili ya mafanikio kuanzia chini na kukua kidogo kidogo. Hata wanaorithi mali pia huweza kufanikiwa sana kwa kuziendeleza.
Siri ya mafanikio makubwa ni kuanza na kidogo na kukikuza hadi kuwa kikubwa. Kwa hiyo hapo ulipo huna ulichokosa, anza leo kutafuta safari yako ya mafanikio kiuhakika na ukifanya hivyo utafanikiwa na kuwa huru.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.