google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 15, 2017

Unajenga na Kubomoa Maisha Yako Hivi…

No comments :
Ni rahisi kwenye maisha yako kuwajibika, kama kweli umeamua kuwajibika na kufanya mambo yanayo kuwajibisha.
Ni rahisi kwenye maisha yako kuendelea na hali ya utoto, kama bado unaendekeza utoto huo na huna dalili hata ya kubadilika.  
Ni rahisi kwenye maisha yako kuendelea kuwa mkomavu wa kifikra na maisha kwa ujumla, kama kweli mambo ya ukomavu ndio unayoyafanyia kazi.
Ni rahisi kujiamini kwenye maisha yako, kama unafanya mambo yanayopelekea  kujiamini kwenye maisha yako pia.
Ni rahisi kuwa na mtu wa sababu na kushindwa kuchukua hatua kama hizo sababu ndizo unaona kwako zinakusaidia sana.

Jenga maisha yako kwa kuchukua hatua sahihi.
Ni rahisi kuendelea kuwa mvivu, kama unaendeleza uvivu usio na maana kwenye maisha yako na kila wakati.
Ni rahisi kuendelea kubaki kwenye umaskini, ukiwa hujaamua kujitoa hasa kupigania kutoka kwenye umaskini.
Ni rahisi kuendelea kuwa mbunifu, kama ubunifu ndio unaotafuta kwenye maisha yako na kuamua kujishughulisha ili kupata ubunifu huo.
Ni rahisi kubaki katika hali yoyote ile, uwe unataka au hutaki ili mradi tu hali hiyo unaifanyia kazi kila mara.
Jiulize, kitu gani unachokifanya sasa kwenye maisha yako? kitu hicho unachokifanya na unakizingatia sana itakuwa ni sehemu ya maisha yako.
Hakuna muujiza, hakuna matokeo ya kushangaza, kile unachokifanya, kile unachokizingatia utakuwa kama kitu hicho.
Matendo yako yanaonyesha wewe utakuwa ni mtu wa aina gani. Vile ulivyo na utakavyokuwa kunaenda sawa na matendo yako.
Washindi wanachukua hatua zinazowafanya wazidi kuwa washindi, wanaoshindwa pia huchukua hatua zinazowapelekea kushindwa.
Usipoteze muda wako kufanya mambo ambayo yatakutoa kwenye ramani ya mafanikio yako, fanya mambo ya kukujenga kimafanikio.
Chochote unachokitaka kwenye maisha yako, usipoteze muda kukisubiri, badala yake chukua hatua za kufanya.
Fanya vitu ambavyo vitakusogeza karibu kabisa na ndoto zako. Fanya vitu ambavyo vitafanya malengo yako yaweze kutimia.
Unaweza kuwa chochote, unaweza kuwa mtu wa mafanikio, unaweza kuwa mtu wa kukubalika, uamuzi wa yote hayo upo mkononi mwako.
Hakuna kinachoshindikana kwako, kumbuka kama nilivyosema, jinsi unavyofanya mambo kwa namna fulani ndivyo unavyojenga au kubomoa maisha yako.
Kwa kifupi unajenga na kubomoa maisha yako kutokana na hatua unazoamua kuchukua ziwe ndogo au kubwa.
Nikutakie kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.