Nov 7, 2017
Dakika Tano Tu, Zinatosha Kukamilisha Mpango Huu Mkubwa Kwako.
Dakika tano ni dakika chache
sana ambazo kila mtu anaweza akazipuuzia na kuona hakuna cha maana unachoweza
kukifanya kwa dakika hizo.
Watu wengi ikiwamo hata
wewe, huona dakika tano ni kidogo na kuamua kuzipotezea hata pale inapotokea
wana umiliki wa dakika hizo tano au chini ya hapo.
Ninachotaka kukwambia ipo
faida na muujiza mkubwa ambao utaupata kwenye maisha yako ikiwa utakubali
kutumia kila dakika tano kubali maisha yako.
Naona unashangaa na
kujiuliza hili linawezekana vipi? Ipo namna ambayo unaweza ukafanya na kubadili
maisha yako kwa kutumia dakika tano ulizonazo.
Tumia muda wako vizuri ukupe mafanikio. |
Kwa mfano, ni dakika tano tu
zinatosha kabisa kukutuliza kutoka kwenye hasira na kutulia hadi kushindwa
kufanya maamuzi ya hasira.
Ni dakika tano pia ambazo
unaweza ukaamua kufanya jambo ulitaka kuriahirisha na kuamua kufanya kwa dakika
tano tu basi.
Ni dakika tano tu
zinakutosha kuanza kuanza kufanya kazi yoyote ambayo ilikuwa na ugumu na mwisho
wa siku ikawa nyepesi.
Hapa unaona kabisa dakika
tano zinaweza zikabadilisha hali fulani ambayo ilikuwa mbovu na ikawa nzuri.
Kwa hiyo hapa ninachoka
unielewe ni hivi,,kwa chochote kile unachotaka kukifanya lakini unaona kuna
ugumu fulani jipe dakaka tano za mwanzo.
Usikubali kuacha jambo hilo
likaishia hewani, kubali kweli kuna ugumu na umechoka na huwezi kufanya, lakini
jipe dakika tano tu za kufanya kidogo.
Inawezekana kuna kitabu
unataka kusoma lakini unaona uvivu, usikubali na wewe ukaacha kabisa, jipe
dakika tano tu za kuanza kusoma kwanza.
Kwa kujipa dakika tano hiyo
itakusaidia kuweza kupata ‘momentum’ mpya
itakayokufanya uweze kusonga mbele kila wakati.
Kwa kutumia dakika tano tu,
utagundua kwamba itakusaidia kutoka kwenye tabia za hovyo zinazo kukwamisha
hadi kwenda kwenye tabia za mafanikio.
Kikubwa unachotakiwa kuelewa
hapa, kujipa dakika tano za kufanya jambo lolote unalolifanya, itakusaidia sana
kukufanikishia mipango yako mingi.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.