Nov 14, 2017
Zijue Mbinu Za Kuijenga Kesho Yako, Yenye Mafanikio.
Hivi ni nani aijuaye kesho yake? Kiimani ukiulizwa swali kama
hili huenda ukakosa majibu sahihi, hii ni kwa sababu wengi wetu hakuna ambaye
aijuae kesho yake. Lakini katika sayari ya upangaji malengo na kanuni ya
mafanikio ni lazima kila mmoja wetu aijue kesho yake.
Hii ni kwa sababu ni lazima kila mmoja wetu aweze kujua ni
wapi ambapo anaelekea katika maisha yake, hii ikiwa na maana ya kwamba kama mtu
ataamua kuyapanga malengo yake katika misingi imara ni lazima kila mmoja wetu
ataijua kesho yake ipoje.
Wakati mwingine ili uweze kuwa bora katika maisha yako ya kila
siku unatakiwa kuweza kujua ni jinsi gani ya kuitengeneza kesho yako. Na mbinu
za kuitengeneza kesho yako mara zote huanza na siku leo, swali la msingi la
kujiuliza ni kwamba unaitumia vipi leo yako ili kuijenga kesho yako?
Kesho yako ya mafanikio inatengenezwa leo. |
Kama utashindwa kuijua leo yako vizuri basi fahamu fika hata
hiyo kesho yako huwezi kuijua pia. Hivyo jambo la muhimu ambalo unatakiwa
kulifanya ni kuhakikisha unaijenga kesho, ni unaijenga tabia ambayo itakufanya
kesho yako iwe ni nzuri. Miongoni mwa tabia ambazo unatakiwa kuziacha ni
pamoja na kuacha kufanya mambo ambayo yatakuwa hayana msaada wowote kwako.
Lakini mara baada ya kuuachana na tabia ambazo zimekuwa
hazikusaidia, lakini jambo jingine ni kuhakikisha unafanya mambo ambayo
yatakufanya wewe uweze kusonga mbele katika maisha yako yako ya kila siku ili
kuijenga kesho yako nzuri.
Hivyo ni vyema ukatafakari kwa makini ni mambo gani ambayo
hayakusaidii, mara baada ya kujua mambo hayo chukua peni na karatasi kisha
yaorodheshe kisha anza kufanya kinyume chake cha mambo hayo.
Kama ulikuwa unatumia muda mwingi kwenye kusoma vitu visivyokuwa
vya msingi basi kuanzia sasa ni vyema ukatenga muda wako katika kusoma vitu
ambavyo vitakusaidia. Kama ulikuwa unachelewa kuamka pasipo na sababu maalum
basi anza pia kufanya kinyume chake.
Mara zote ili uweze kuijenga kesho yako unachotakiwa kufanya hakikisha
ya kwamba unafanya mambo kwa uhakika na ustadi wa hali juu. Kila unachokifanya
ni vyema ukatumia ile kanuni ya kwenda mbele zaidi.
Kama ni biashara ni lazima ujifunze kufanya vitu ambavyo
vitakufanya uweze kusonga mbele, achana na tabia ambazo zimekuwa hazileti
matokeo chanya.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku njema na
mafanikio mema.
Ndimi ; BENSON CHONYA
0757-909942.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.