Nov 3, 2017
Hata Kama Mambo Yanakwenda Vibaya, Fanya Hivi...
Ni rahisi sana kuwa na
hasira, kukatishwa tamaa na hata msongo wa mawazo. Hiki ni kiu ambacho kila mtu
anaweza akawa nacho kwenye maisha yake.
Nikiwa na maana kila mtu akikasirishwa,
anaweza akakasirika sana au mtu akikatishwa tamaa anaweza akakata tamaa pia sana.
Lakini yote hiyo haiwezi
kusaidia kitu. Busara na ukomavu wako wa kimaisha unakuja pale hasa unapokwenda
kinyume na mambo hayo.
Ni kweli unaweza ukawa umekasirishwa
na ukatamani upige mtu sana, sasa je, kwani ni lazima ifike mahali ukakakasirika
kwa kiasi hicho?
![]() |
Usifanye hali mbaya ikawa mbaya zaidi. |
Ni kweli unaweza ukawa
umekatishwa tamaa, lakini kwa wewe haina haja kuendelea kufanya mambo ambayo
yanakukatisha tamaa zaidi.
Unachotakiwa kufanya au
kujifunza ni kuweza kugeuza mambo ya hovyo na yakawa bora zaidi hata kama
imetokea hali ya kukasirishwa au kukatishwa tamaa.
Kufanya hali mbaya ambayo
tayari naweza kusema umeshapewa na ikawa ni nzuri, huo ni ukomavu wa hali ya
juu utakaokufanya uishi vizuri sana duniani.
Mtu amekuuzi sana na wewe huhitaji
kuendelea kufoka au kuumia zaidi. Unatakiwa kutuliza akili yako na kufanya
mambo ili yawe mazuri.
Kufanya mambo yawe mazuri
hasa pale yanapokuwa yameharibika ni kitu ambacho unatakiwa ujifunze nacho sana
karibu kila siku.
Kila siku na kila wakati
endelea kuweka juhudi za kuwa mtu chanya, mpaka maisha yako yalete utofauti
mkubwa na kwa wengine.
Ni watu wachache sana ambao
wako tayari kubadilisha hali mbaya ya msongo wa mawazo walionayo, kukatishwa
tamaa na kukasirishwa kuwa nzuri.
Wengi wakikasirishwa na wengine
hukasirika na kukasirisha zaidi. Hivyo, unatakiwa usiwe miongoni mwao.
Unatakiwa uwe mtu wa kubadilisha hali.
Kufanya hali yoyote iwe bora
ni zoezi ambalo unaweza ukalifanya karibu kila siku kwenye maisha yako pale
ambapo unakuwa unaona mambo hayajakwenda sawa.
Unatakiwa uelewe hili, pale
mambo yako yanapokwenda hovyo, fanya mambo hayo yawe bora. Jitahidi kubadili
hali hiyo kwa busara na ikawa bora.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.