google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 20, 2017

Mambo Ya Kukumbuka Sana Wakati Unatafuta Mafanikio.

No comments :
Yapo mambo ya msingi ambayo kila wakati unatakiwa uyakumbuke unapotafuta mafanikio yako. Kwa nini unatakiwa kuyakumbuka mambo hayo, hiyo yote ni kwa sababu ndio kama msingi na nguzo ya kufikia mafanikio yako.
Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutoyajua au kutoyakumbuka kabisa mambo hayo na mwisho wa siku hujikuta wakipotea na kushindwa kufikia mafanikio yatakawayo kimaisha.
Kupitia makala haya nataka nikukumbushe mambo ya msingi sana ambayo unatakiwa kuyakumbuka wakati unatafuta mafanikio. Naamini utajifunza na itakusaidia kuchukua hatua ya kufanikiwa kwa kuyajua mambo haya tena.
1. Jipe muda wa kufanikiwa.
Mafanikio ni kitu ambacho hakitokei mara moja tu. Mafanikio yanaenda hatua kwa hatua. Si kwa sababu eti kuna jambo umepanga kulifanikisha basi ulifanikishe leo leo, kama ni hivyo basi huo utakuwa ni uongo mkubwa sana.
Unatakiwa ujipe muda wa kufikia mafanikio yako. Acha kuangalia njia za kutaka kujipatia utajiri wa haraka. Unatakiwa kuweka juhudi kila siku. Hata Roma kumbuka haikujengwa kwa siku moja na mafanikio pia yanataka mchakato vivyo hivyo.
Wakati mwingine inaweza ikakuchukua miaka 5, 10, 17 na hata 20 ili kuweza kufikia mafanikio makubwa uyatakayo. Usishangae huo ndio ukweli,  ila kama wewe wa kutaka mafanikio makubwa na ya haraka, jiandae mafanikio hayo yatakupoteza rafiki.

2. Fanya kile unachokiamini kitakupa mafanikio.
Usifanye hata siku moja kosa kwa kuamua kufanya kitu ambacho moyoni mwako unaona hakikupi mafanikio. Fanya kile ambacho unaamini kinakupa mafanikio, hata kama kitu hicho kinadharaulika sana kwa wengi.
Kwa kufanya kile kitu ambacho unaamini kitakupa mafanikio, naamini utaweka juhudi sana hadi kuweza kufikia mafanikio yako makubwa. Ila kama unataka kushindwa kabisa fanya kitu ambacho unaamini hakikupi mafanikio, utajuta.
3. Fanya kile unachokipenda.
Hakuna mafanikio makubwa utakayoweza kuyapata kwa wewe kufanya kile kitu usichokipenda. Najua hili tumeliongelea sana hapa, lakini nakukumbusha ili kufanikiwa unatakiwa kufanya jambo unalolipenda kwanza.
Ukiwaangalia watu wote wenye mafanikio wanafanya vitu wanavyovipenda kwani huko ndiko mafanikio makubwa yanapopatikana yaani inapotokea chanagamoto ni rahisi kuweza kupambana nayo mpaka kieleweke.
4. Boresha kile ukifanyacho kila siku.
Haijalishi kile unachokifanya ni bora kiasi gani, lakini maboresho kwa kile ukifanyacho ni muhimu sana, kama hautaweza kuboresha kile unachokifanya itafika mahali utakwama na hautaweza kusonga mbele sana.
Boresha kuanzia leo biashara yako, uandishi wako, akili yako kwa kujisomea kila siku ili uweze kusonga mbele. Kitu chochote ambacho hakina maboresho mafanikio yake ni ya muda mfupi sana na itafika wakati mafanikio hayo hupotea.
5. Jifunze kutokana na makosa yako.
Kwenye maisha hakuna kitu kinachoitwa ushindi wa moja kwa moja. Inabidi ifike mahali ukubali kujifunza kutokana na makosa pale unaposhindwa. Ukijifunza tu kutokana na makosa hiyo itakuwa ni fursa bora kwako ya kukusaidia kuweza kusonga mbele.
Naamini kwa kujifunza mambo hayo kuna kitu ambacho umetoka nacho na kimekusaidia kuweza kuchukua hatua ya kuweza kusonga mbele. Fanyia kazi hayo na ukumbuke kila unapotafuta mafanikio yako.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.