Nov 18, 2017
Ijue Msingi Ya Kuwa Mbunifu.
Katika
maisha yako yote ambayo unayaishi hapa dunia basi tambua ya kwamba bila kuwa mbunifu
basi utaendelea
kuungua na jua maisha yako yote, nasema hivyo nikiwa na maana ya kwamba
asilimia 99.99 ili uweze kupiga hatua za kimafanikio kila wakati katika maisha yako ni lazima uwe mbunifu.
Ubunifu
ndio nguzo nambari moja ambayo itakufanya wewe kuweza kufanikiwa, ikiwa
hautajenga misingi ya ubunifu katika jambo lolote ambalo unalifanya basi ni
kwamba utaendelea kuishi maisha ya kawaida na matokeo ambayo utayapata nayo
tayakuwa ni ya kawaida tu.
Kwa sababu
katika karne hii kwa asilimia kubwa kitu
ambacho unakifanya wewe kwa asilimia
kubwa ni lazima kitafanana na mtu mwingine, kama ndivyo hivyo basi ikiwa
mfanano wa vitu unazidi kuongezeka swali la msingi ambalo unatakiwa kujiuliza ni,
hivi natajitofautishaje na wenzangu?
Majibu
ya swali hilo ni kwamba ili kujitofautisha na wengine unachotakiwa kufanya ni
kuhahahakikisha ubunifu unahusika kwa asilimia kubwa. Mtu mwingine anaweza kuja
kifua mbele akaniuliza sasa afisa mipango huo ubunifu ni nini?
Pasipo
kuona haya endapo niutaulizwa swali kama hilo jibu ambalo nitampa nitamwambia,
ubunifu ni kuongeza thamani kwa kitu ambacho unakifanya, aidha kama utashindwa kuongeza thamani basi utakiwa
kuunda kitu kipya.
Katika
swala kuunda kitu kipya hapa ndipo pamekuwapo na tatizo fulani kwa sababu watu
wengi wanapenda sana ganda la ndizi kuteleza, kwa maneno mengine
tunaweza kusema akili zao zimeganda hasa katika suala la kufikiria wao wamekuwa
wanapenda sana kufanya ‘copy & paste.’ Kufanya hivyo ni kujipoteza
mwenyewe hivyo unachotakiwa kufanya ni kwamba lazima uwe na misingi ya kubuni
kitu cha kwako.
Pasipo
kupoteza kusudio la mada yangu ya siku ya leo, niliona ni vyema niianze na
utangulizi huo ili uelewe maana ya ubunifu. Mara baada ya kufahamua maana ya
ubunifu basi naomba japo kwa dakika chache tuangalie misingi ya ubunifu kama ifuatavyo.
1. Fanya kitu Unachokipenda.
Ukitaka
kuwa mbunifu katika eneo lolote lile , kwanza ni lazima uhakikishe unafanya
kitu ambacho unakipenda. Ukifanya kitu ambacho unakipenda kwa asilimia zote,
upo uhakika wa asilimia zote kwamba ni lazima utakuwa mbunifu ili kuwashinda
washindani wako wanakuzunguka.
2. Wekeza muda katika kuwaza na kutenda
jambo hilo.
Ili
uweze kuwa mbunifu katika jambo ambalo unalifanya jambo jingine ambalo
unatakiwa kulizingatia ni kwamba ipo haja kubwa sana ya kuwekeza muda mwingi
katika kuliwaza na kulitenda jambo hilo. Hivyo kwa kuwa umeamua kuyasaka
mafanikio kwa udi na uvumba huku ukiamini ya kwamba ubunifu ndiyo ambao
utakusaidia kuwa hivyo basi hakikisha ya kwamba unajipanga kikamilifu kuweza
kujitoka kwa kuwekeza muda wako mwingi ili kuweza kulitimiza jambo hilo.
3. Jifunze vitu vipya vinavyoendana na
jambo lako.
Jambo
jingine ambalo litakufanya wewe uweze kuwa mbunifu ni kwamba ni lazima uhakikishe
ya kwamba kila wakati huchoki kujifunza vitu vipya ambavyo vinaendana na jambo
hilo. Sambamba na hilo kwa kuwa binadamu kwa asilimia kubwa kuna uwezekano
mkubwa sana wa kile alichojifunza kuweza kusahau, hivyo kwa kile ambacho
unajifunza ni lazima uhakikishe ya kwamba unakiandika na uwe unakipitia mara
kwa mara ili usikishau.
4. Jiulize maswali mara kwa mara.
Jambo
la mwisho kati ya mengi yahusuyo somo hili ni kwamba kila wakati ni lazima uwe
ni mtu wa kujiuliza maswali ya mara kwa mara. Moja kati ya swali muhimu ambalo
unapaswa kujiuliza wewe katika misingi hii ya ubunifu ni, Je hivi nikifanya jambo
hili nitapata faida gani?
Mpaka
kufikia hapo sina la ziada nikutakie ubunifu mwema na siku njema.
Ndimi: Afisa Mipango ; Benson Chonya
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.